TLS YAWAKABA KOO VIGOGO WA POLISI ARUSHA , YAAPA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YAO KWA KUBAMBIKA RAIA MAKOSA YA UONGO,PIA KUWAFIKISHA TUME YA MAADILI YUMO RPC NA OCD MATAGI HAWAPONI!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Sakata la kukamatwa na  kushikiliwa na polisi kwa wakili Valerian Kamala limechukua sura mpya mara baada ya Chama cha Mawakili Tanganyika TLS, Tawi la Arusha,kutoa tamko kali la kulaani kitendo hicho na kuazimia kuwashtaki mahakamani vigogo wa polisi Mkoani hapa wakiongozwa na Kamanda wa polisi Justine Masejo na Mkuu wa Polisi wilaya OCD Georgina Matagi ambao watashtakiwa kwa makosa yao wenyewe.


Wengine watakaoshtakiwa ni Mkuu wa Polisi Nchini,IGP Camilius Wambura, Mkuu wa upelelezi wa mkoa(RCO), Mkuu wa kituo cha polisi cha kati OCS Sotel,na mwendesha mashtaka wa Mkoa DPP, pamoja na Raia wa Kigeni aliyedai kupigwa .

No

Akitoa tamko hilo leo mbele ya waandishi wa habari katika kituo cha haki jumuishi Mkoani hapa , mwenyekiti wa TLS kanda ya Arusha, George Njooka alisema hatua hiyo imekuja kufuatia kukamatwa kwa wakili huyo na kubambikiwa makosa ya uongo ya wizi wa kutumia silaha na kunyimwa dhamana iliyopelekea kusota mahabusu kwa siku tatu  bila dhamana kabla ya kuachiwa jana jioni.


"Lazima tuwaonyeshe sisi na Polisi tunatofauti wasituchukulie poa,hatutatoa matamko tena tutaongea kwa vitendo,hatutajali wewe ni Taasisi gani na unacheo kipi ilimradi umevunja cheria tutashughulika na wewe appendicular"Alisisitiza Njooka.


Alisema makosa watakayowashtaki nayo  ni Kumshikilia wakili kinyume cha sheria kwa makosa ya yasiyomhusu,Kumbambikia kesi ya uongo na kumnyima dhamana kinyume cha sheria.


"Tumepanga kukomesha tabia hii ovu ya jeshi la polisi kuwabambikia raia makosa ya uongo kwa matakwa ya mtu mmoja ,tumeamua kuwashtaki  kwa fidia kwa makosa yao wenyewe ili iwe fundisho na rais amekuwa akikemea tabia ya jeshi hilo ila baadhi yao hawataki kukoma"


Aidha mawakili hao pia wameazimia kuwashtaki vigogo hao wa polisi tume ya maadili kwa kukosa weledi katika utendaji wao wa kazi na wamekubaliana kufanya mgomo wa uwakilishi mahakamani kwa watuhumiwa hao wa polisi wakati watakapoitwa mahakamani.

"

Jana tulisema tutawafungua kesi mahakamani,tumefungua kesi mahakama kuu na ikasajiriwa  namba 2297 ya mwaka 2025 na ikapangiwa jaji wa kutusikiliza ili waitwe na waieleze mahakama kwanini wanamshikilia wakili na kumnyima dhamana, walizani tunatania tumefanya hivyo na leo kesi ilipangwa kusikilizwa saa nane mchana lakini hawakuja baada ya jana kumwachilia wakili Kamal
a"


Tayari Mwenyekiti huyo ameunda jopo la Mawakili kushughulikia kuandaa mashtaka hayo na kuya fikisha mahakamani kwa ajili ya kusajiriwa kwa kesi hiyo itakayotikisha hapa nchini.


Awali jeshi la polisi kupitia kamanda wa polisi Mkoani hapa, Justine Masejo alinukuliwa kupitia taarifa ya jeshi hilo kuwa wanamshikilia wakili huyo wa kujitegemea pamoja na dereva bodaboda,Benjamini Paul 19,wakihusishwa na tukio la kushambuliwa kwa raia wa Kigeni wa nchini Afrika kusini, Zuzan Merry Shawe mkazi wa Block C 1Njiro na watu wanaodaiwa kutumwa na wakili huyo.

Wakili Valeriani Kamala baada ya kuachiliwa na polisi ,akiwashukuru mawakili wenzake 

Akiongea mara baada ya kuachiwa kwa dhamana jana wakili Valerian Kamala,aliwashukuru Mawakili wenzake kwa umoja wao na sauti zao zimesaidia kupatiwa dhamana ambayo hapo awali alikataliwa na kukaa mahabusu.


Alisema jeshi hilo lilimwachia huru kwa dhamana jana na kutakiwa kufika leo kituoni wakati upelelezi wa shauri hilo hilo ukiendelea.








Ends...



Post a Comment

0 Comments