TOZO MPYA ZAIBUA TAHARUKI SEKTA YA UTALII TATO YALIA NA TAWA YAMWANGUKIA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI,YATAHADHALISHA ATHARI ZA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA UTALII .

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


CHAMA cha Mawakala wa Usafirishaji Watalii nchini Tanzania (TATO)kimepinga Matumizi ya  tozo Mpya kwenye Mapori Tengefu zilizotangazwa hivi karibuni na Mamlaka ya Usimamizi wanyama pori Tanzania (TAWA) kupitia gazeti la serikali na kudai kwamba mabadiliko hayo yatapunguza idadi ya watalii kuingia Nchini.

Akiongea na waandishi wa habari leo January 23,2025 katika ofisi za Tato Jijini Arusha,Makamu mwenyekiti wa Tato,Henry Kimambo,aliomba serikali kusitisha mabadiliko hayo ya Tozo kwenye mapori tengefu, wakihitaji ushirikishwaji zaidi kwa wadau wa sekta hiyo ili kuondoa malalamiko na usumbufu kwa watalii wanaofika kutalii nchini Tanzania.

"Lengo la Mkutano huu ni kufikisha kilio chetu kwa serikali kutokana na taharuki iliyojitokeza katika sekta ya utalii baada ya  kutangazwa mabadiliko ya Tozo mpya katika mapori Tengefu ambazo zitaumiza watalii ambao walishalipia safari za kuja nchini Tangu Mwaka jana"

Kimambo alisema Tozo Mpya ambazo zimeanza kutumika  tangu January 17,Mwaka huu , zimeleta usumbufu mkubwa kwa baadhi ya watalii, kampuni za Utalii na kwa wadau wengine wa sekra hiyo hapa nchini .

Athari zingine zilizotokana na Kupanda kwa Tozo hizo ni kupungua ama kuondoka kwa watalii katika maeneo ya Mapori ya akiba, Mapori Tengefu na hifadhi za Jamii (WMA) zinazosimamiwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania TAWA.

Alisema mabadiliko ya kanuni hizo za tozo yamekuja ghafla bila kushirikishwa akisema suala hilo walishakitana marakadha kulijadili lakini kabla ya kufikia mwafaka  wameshangaa limetoka kwenye portal ya wizara na kuanza kutumika kama kanuni rasmi.

Alisema suala hilo lisipoangaliwa kwa kina litapunguza watalii hasa wale ambao tayari walikwisha fanya taratibu za malipo na kuanza kupanga safari za kuja kutalii nchini Tanzania tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Kimambo amewaambia wanahabari kuwa kuendelea kutumika kwa kanuni hizo mpya kutasababisha hasara kwa makampuni ya utalii, usumbufu kwa watalii, makampuni na madereva waongoza watalii pamoja na mdororo mkubwa wa kupungua ama kuondoka kwa watalii katika maeneo ya mapori tengefu na hivyo kusababisha athari za kiuchumi na kijamii kwa wakazi wanaozunguka maeneo hayo tengefu.

Alisema kuwa mabadiliko hayo yalipaswa kishirikishwa kwa wadau wa sekta ya utalii ili kuondoa mkangamyiko ambao umeamza kujitokeza na kuleta madhara.

Kimambo alisema kulingana na tozo mpya, madereva watalii sasa wanapaswa kulipa ada ya shilingi 41, 300 kutoka shilingi 8,260 ya awali, tozo ya gari itakuwa 23,600 kutoka shilingi 17,700 huku Mtalii akilazimika kulipa Shilingi 70,800 kama tozo ya kiingilio kutoka shilingi 30, 149 za awali huku tozo nyingine ya Bednight ikiwa ni shilingi 59,000 kutoka shilingi 45, 223 kwa mtalii huku dereva wake akitakiwa kulipa shilingi 23,600 kutoka ile ya awali ya shilingi 5900.

Kimambo aliomba wizara ya Maliasili na Utalii kuchukua hatua za Maksudi haraka na kusitisha mara moja Matumizi ya Tozo mpya na kuruhusu mchakato wa pamoja wa kujadili Tozo hizo ufanyike hatua ambayo itasaidia kuondoa mkanganyiko huo ambao umeleta taharuki na usumbufu mkubwa kwa watalii.

Ends..  


Post a Comment

0 Comments