Na Joseph Ngilisho ARUSHA
TAASISI ya Dini ya Kiislamu ya Twarika,imetangaza kufanya chaguzi katika taasisi zake zote hapa nchini ili kupata viongozi wenye uwezo na weledi wa kuongoza taasisi hiyo kongwe hapa nchini kuanzia ngazi ya Taifa , Mkoa hadi wilaya katika mikoa yote Tanzania.
Akiongea katika Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo mapema leo Jumamosi, January 11,2025,uliofanyika makao makuu ya Twariqatul Qadiriyya Arraziqiyya Al-Jaylanyya Al-kaylaniya Mkoani Arusha,kiongozi wa Twarika Tanzania, sheikh Mubaraka Salim,alisema kuwa mkutano huo umelenga kuteua viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa na wilaya ili kuziba nafasi zilizowazi.
Alisema kwa kuanzia watafanya chaguzi katika mikoa mitano ya Arusha Manyara,Singida,Shinyanga na Mwanza,na baadaye katika mikoa ya Dodoma ,Dar Es Salaam ,Morogoro, Tanga na Kilimanjaro.
"Rai yangu kwa viongozi watakaoteuliwa kuwa waadilifu,wakaimarishe Zawiya Zote,watengeneze mpango kazi wa kuwa na kipato cha Kujiendesha ,kuacha mazoea na kuwa na hofu ya mungu"
Naibu katibu Mkuu wa Twarika Taifa,Sheikh Haruna Husein alisema wao kama viongozi wapya walioteuliwa hivi karibuni ngazi ya Taifa wanajukumu la kuimarisha Taasisi hiyo kwa kuzunguka mikoa yote nchini kuhamasisha chaguzi na kuteua viongozi makini watakaoshirikiana na serikali kulinda amani ya Taifa.
Aidha sheikh Haruna alimpongeza rais Samia Suluhu Hasani kwa kuendelea kuthamini mchango wa taasisi za za dini katika kuimarisha amani hapa nchini na kumwomba kuipa kipaumbele taasisi hiyo ya Twarika kama taasisi kongwe yenye zaidi ya miaka 80 hapa nchini.
Aliwataka viongozi wanaoteuliwa kuacha kufanyakazi kwa mazoea kujiepusha na makundi yasio na tija,kuheshimiana na kuheshimu viongozi wa serikali waliopo madarakani.
Aidha naibu katibu huyo aliiomba serikali kutambua mchango wa taasisi hiyo kongwe yaTwarika katika kukemea maovu , kuhamasisha maendeleo na kuhubiri Amani ndani na nje ya Taifa letu
"Tangu tumeteukiwa tunaenda na kauli mbiu yetu inayosema acha mazoea badilika ,tukiwa na maana kwamba usikae kwenye nafasi kwa kutafuta cheo ,simamia kwa uadilifu nafasi uliopewa "
Aidha amekipongeza kituo cha Mikutano cha kimataifa Arusha Aicc kwa kukubali ushirikiano na taasisi hiyo ya dini ikiwemo kuahidi kutatua baadhi ya changamoto na kueleza kuwa nimwanzo mzuri wa dini hiyo kuwa na ukarinu na taasisi za umma
Awali mwenyekiti wa Twarika mkoa wa Arusha,alisema Taasisi ya Twarika ina malengo makuu ya kujenga mahusiano baina ya taasisi hii na taasisi zingine ndani ja nje ya nchi na haitajihusisha na masuala ya siasa na itashirikiana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Bakwata.
Ends..
0 Comments