SHIRIKA LA TANAPA LATUNUKIWA CHETI CHA UBORA WA MIFUMO KUTOKA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA ISO ,TANAPA YASEMA IMEAMINIKA KIMATAIFA MAPATO YAONGEZEKA KILA MWAKA!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


SHIRIKA la hifadhi za Taifa Tanapa, limekabidhiwa cheti cha Umahiri wa mifumo yake ya utoaji wa huduma kwa viwango vya juu ikiwa ni mara ya pili kupokea cheti hicho kutoka  Shirika la viwango Tanzania (TBS).
Akikabidhi Cheti hicho kitakachodumu kwa miaka mitatu ,Mkurugenzi Mkuu wa shirika la viwango Tanzania Dkt, Ashura Katunzi alisema shirika hilo limepokea vyeti Saba ambapo vingine ni miongoni mwa vituo ishirini na Moja walivyo navyo huku akisisitiza mashirika mengine kuwa na uweredi katika utoaji huduma .

Alitoa rai kwa Tanapa kuhakikisha hithibati hiyo inaleta manufaa makubwa ikiwemo kuongeza ujasiri kwa wateja na watalii mnaowahudumia na wale  wanaopata huduma za Shirika la Tanapa. 

"Hongereni sana Tanapa kwa kupata hithibati hii bila shaka mtaendelea kuidumisha kwa sababu mmeshapata uzoefu kupitia mzunguko wa kwanza, nitoe wito kwa Taasisi zingine na sekta  binafsi na za umma, kuthibitisha mifumo yao ya kusimamia  ubora kwa kuitumia TBS ambayo inacheti cha kimataifa  cha ukahiri katika huduma hii"

Aidha dkt Ashura alisema utoaji wa cheti hicho umekuwa hauzingatii ukubwa au udogo wa shirika hivyo ni vyema taasisi nyingine za umma zithibitishe mifumo yao ili kujiweka katika viwango Bora vya utoaji huduma 

Kwa upande wake kamishna wa uhifadhi na maendeleo ya biashara Tanapa (Dcc) ,Massana Mwishawa alisema shirika hilo litahakikisha kinaendelea Kutoa huduma zenye ubora na viwango vya hali ya juu na vilivyowekwa Kimataifa .

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu idadi ya watalii na mapato yanaongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika mwaka wa fadha 2021/22 jumla ya watalii walikuwa 997,873 na mapato yalifikia sh.174,715,158,493.75.Mwaka 2022/23 jumla ya watalii walikuwa 1,670,437 na mapato yalikuwa sh,337,424,076,896.29.

Alisema mwaka 2023/24 jumlamya watalii walikuwa 1,862,540 na mapato yalikuwa sh,410,903,648,082.30 na katika kipindi cha miezi sita julai hadi desemba 2024/25 watalii wapatao 1,146,438 wametembea hifadhi ya taifa na mapato ya sh,milioni 325,146,978,076.63 yameparikana.

Alisema mfumo huo umesaidia kutambua hitaji la wateja mapema na kuyaingiza kwenye mipango yao na imesaidia kujitangaza kimataifa.

Miongoni mwa vituo vilivyopokea vyeti hivyo ni pamoja na hifadhi ya Mkomanzi ambapo Emmanuel Mwinara ambaye ni kamishina msaidizi wa uhifadhi na mkuu wa hifadhi hiyo alisema kupewa cheti hicho kwa mara ya pili inawasaidia kujenga imani kwa Umma katika utoaji wa huduma Bora . 






Ends..




Post a Comment

0 Comments