Na Joseph Ngilisho ARUSHA
SIKU moja Mara
Akiongea na vyombo vya habari mapema leo, January 26,2025, Mwenyekiti wa TLS tawi la Arusha, George Njooka alisema kuwa chama hicho kimeazimia kuwafungulia mashtaka vigogo wa Polisi Mkoani Arusha kwa kumbambikiza kesi ya uongo ya wizi wa kutumia silaha wakili huyo ambaye ni mwana chama wao wa TLS.
"Tutakao wafungulia mashtaka ya fidia ni Mkuu wa kituo cha Polisi cha cha kati ,OCS SOTEL,Mkuu wa Polisi wilaya OCD , Georgina Mataji na Kamanda wa Polisi Mkoa RPC Justine Masejo "Alisema wakili Njooka.
Aidha alisema kuwa chama hicho kimeazimia pia kuandika maombi maalumu ya dharura ya kuiomba mahakama kulishurutisha jeshi la polisi kumpeleka mtuhumiwa mahakamani hapo kesho January 27 ili kusikiliza kesi yake na wamejipanga kwa pamoja kumwakilisha mtuhumiwa huyo mahakamani.
"Sisi Chama cha Mawakili wa TLS tawi la Arusha tunalalamikia kukamatwa kwa wakili mwenzetu wakati akitekeleza majukumu yake ,tumeazimia kupeleka maombi ya dharura mahakamani ili wakili aweze kufikishwa mahakamani kesho kwa hati ya dharura"
"Azimio la pili ni kuwashtaki kwa fidia viongozi wa jeshi la polisi kwa kosa la kumshikilia pasipo halali wakili, ambao ni Afande Adamu,(OCD) Georgina Mataji,afande (RPC) Justine Masejo,pia tutampeleka mahakamani mama wa kizungu kwa kutoa taarifa za uongo "
Awali jeshi la polisi kupitia kamanda wa polisi Mkoani hapa, Justine Masejo alinukuliwa kupitia taarifa ya jeshi hilo kuwa wanamshikilia wakili huyo wa kujitegemea pamoja na dereva bodaboda,Benjamini Paul (19),wakihusishwa na tukio la kumshambulia raia wa Kigeni wa nchini Afrika kusini, Zuzan Merry Shawe mkazi wa Block C 1Njiro na watu wanaodaiwa kutumwa na wakili huyo.
Taarifa ya RPC Masejo ilidai kuwa tukio hilo lilitokea nyumbani kwa raia huyo wa kigeni January 21,mwaka huu,majira ya saa 3 asubuhi na kwamba uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa mawakili alihoji hatua ya jeshi hilo kushindwa kumkamata mhusika mkuu wa tukio hilo aliyeenda kumkamata mzungu kwenye nyumba na kumshusha chini ,aliyemtaja kwa jina moja la ABDUL .
Aidha mwenyekiti Njooka alisema TLS inalaani kitendo cha kumkamata Wakili huyo kwa makosa ya shambulio la aibu na kisha kumbadilishia mashtaka juu kwa juu na kumbambikiza mashtaka ya wizi wa kutumia silaha na pia walikubaliama kuandamana kituo cha polisi kwenda kumwona wakili huyo jambo ambalo liligonga mwamba baada ya kukumbana na kizinguti cha askari kuwazuia.
Pia wamekubaliana kupeleka mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ili kuondokana na msuguano wa mara kwa mara na jeshi la polisi ambao imepelekea kushusha thamani ya taaluma yao.
Baadhi ya mawakili wakichangia hoja juu ya tukio hilo, wakili Emmanuel Mvuka alienda mbali zaidi na kutaka mawakili hao kugomea shughuli za mahakama hadi hapo mwafaka juu ya madai yao na jeshi la polisi yatakapopatiwa mwafaka.
Ends...
0 Comments