RAIS MWINYI: KILA MWANANCHI KULIPWA FIDIA ANAYOSTAHILI.
By Ngilisho Tv
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali itamlipa kila Mwananchi haki yake na hakuna Mwananchi atakae sononeka kwa Kukosa fidia.
Rais Dk.Mwinyi ametoa agizo la Kila Mwananchi Kulipwa kile anachotaka ikiwa Malipo ya Fedha au Nyumba.
"Kila Mwananchi atalipwa kwa kile anachotaka wa fedha alipwe fedha na anaetaka nyumba atalipwa nyumba" amesisitiza Dk.Mwinyi
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka Jiwe la Msingi Mradi wa Nyumba 370 za Maakazi ziliopo Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni Nyumba za fidia kwa Wananchi walioathirika na Ujenzi wa Barabara katika Eneo la Mangapwani ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani.
Rais Dk.Mwinyi amewahimiza Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kuchangamkia Fursa za Kiuchumi zitakazokuwepo kwenye Miradi mikubwa ya Maendeleo iliyomo Mkoani humo .
Akizungungumzia Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani ameeleza kuwa tayari Mkandarasi amelipwa malipo ya awali na ameanza kazi za upimaji wa sampuli za udongo katika eneo hilo kuelekea kuanza ujenzi.
Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inakusudia kujenga Uwanja Mkubwa wa Michezo( Football Academy) katika Mkoa wa Kaskazini Unguja utakaokuwa na Viwango vya Kisasa.
Rais Dk Mwinyi ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi ,Wakala wa Majengo ZBA kwa Usimamizi mzuri uliofanikisha Ujenzi wa Nyumba hizo pamoja na Mkandarasi wa Ujenzi huo Kampuni ya ORKUN ya Uturuki.
0 Comments