Na Joseph Ngilisho ARUSHA
RAIA wa kigeni na Mkazi wa Engutoto jiji Arusha , Zuzan Merry Shawe(75) mwenye uraia wa nchi ya Afrika kusini,amenusurika kuuawa na kundi la watu wanaodaiwa kutumwa kwa lengo la kumteka na kumtoa ndani ya nyumba anayoishi kwa madai ya kushindwa kulipa kodi.
Tukio hilo limetokea juzi January 21,Mwaka huu, majira ya saa tatu asubuhi ambapo watu hao zaidi ya 20 wakiwa na mapanga ,Nyundo na Nondo walimvamia Nyumba ya Raia huyo wa kigeni na kuanza kumshambulia kwa silaha hizo na kumjeruhi kwa kumpiga nyundo kichwani na kumvunja mkono wa kulia kwa kumpiga na nondo huku wakiwavungia ndani mbwa wake wa ulinzi.
Katika tukio hilo watu hao pia walimpora simu zake tatu za Mkononi pamoja na za wafanyakazi wake na walivamia chumbani kwake na kuiba fedha kiasi cha sh,milioni 7 pamoja na Dola 2000 za kimarekani.
Akiongea na waandishi wa habari nyumbani kwake,Raia huyo wa kigeni alisema kuwa majira ya asubuhi walifika watu asiowafahamu wakiwa na pikipiki sita walizokuwa wamepakizana watatu na kuvamia nyumba hiyo ambayo amepangisha na ameishi hapo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Alisema watu hao walikuwa na Kiongozi wao waliokuwa wakimwita kwa jina moja la ABDUL ambaye alikuwa akiwashurutisha wenzake kwa kuwapiga akiwataka kumtoa mzungu ndani ya nyumba hiyo kwa nguvu na kuondoka naye .
"Nilikuwa chumbani kwangu nikasikia kelele, dada wa kazi alikuja na kuniambia kunatatizo kubwa nje ,ndipo nilipofunga mlango wangu kwa komeo na baada ya muda mfupi nilisikia mlango wangu ukivunjwa na watu waliingia chumbani na kunikamata walinipeleka bafuni na kuanza kunipiga na nyundo kichwani na baadaye waliniburuza kutoka gorofani hadi chini getini nikiwa sina nguo huku wakiniambia nitoke ndani ya nyumba kwa sababu nadaiwa kodi na baada ya kunitoa wengine walibaki ndani ya chumba changu na kukipekua "
Hata hivyo mmoja ya mfanyakazi wa Suzan,Ayubu Malolo alisema majira ya saa tatu walifika watu wakiwa na pikipiki sita wakiwa na mapanga na Nyundo na kumwambia ..."kwanini mnaishi hapa bila kulipa kodi, walinitaka niwapeleke juu kwenye chumba cha bosi wangu,kiongozi wao aitwaye ABDUL alitangulia na kwenda kuwafungia Mbwa kwa komeo waliokuwa wakipiga kelele ili wasitoke,nilipofika juu na kuwaonesha chumba cha Bosi wangu waliniweka chini ya ulinzi na kuanza kuvunja mlango na kuingia chumbani "
"Nilimsikia Kiongozi wao akisema mtoeni huyo mzungu walianza kumburuza akiwa uchi hadi getini huku wakimpiga na nyundo kichwani,walipofika getini walikuta watu wamejaa ndipo walipoamua kumtelekeza na kukimbia"
Alifafanua kuwa yupo hapa nchini kwa ajili ya kufuatilia mirathi ya marehemu mume wake aliyefariki miaka miwili iliyopita na wameishi katika Nyumba hiyo kwa zaidi ya miaka 20 akiwa mpangaji aliyepangishwa na Irene Sianga anayeishi nchini Uingereza kwa makubaliano ya kumlipa kiasi cha dola 800 kila Mwezi sawa na zaidi ya sh,milioni 2 za kitanzania ambazo amekuwa akilipa kila Mwezi.
Hata hivyo alisema hadi sasa hakuna fedha anayodaiwa na mara ya Mwisho amemlipa mwanzoni mwa mwezi huu kwanza .
Mmoja ya mawakili wa kampuni ya uwakili ya HAKIKA ,Valerian Kamala alisema walipata malalamiko kutoka kwa mteja wao wa kampuni ya Life Trust Ltd inayomilikiwa na familia ya Sianga akiwemo Kasian na Irene na wengine ambao ndio wamiliki wa nyumba aliyopangisha Zuzan, (raia wa Kigeni) kuwa Zuzan anadaiwa kodi kiasi cha dola 10,800 ambazo hajalipa tangu mwaka 2023 na kuamua kumwandikia notice ya kuondoka kwenye nyumba.
Hata hivyo wakili Kamala alikanusha kufahamu mpango wa kutumia wahuni kwenda kumteka raia huyo wa kigeni na kumtoa ndani ya nyumba hiyo kwa nguvu ikiwa ni njia moja wapo baada ya kukaidi kutoka licha ya notice ya siku saba waliompatia January 7,mwaka huu na kudai kuwa hao ni waharifu kama waharifu wengine na wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa hafahamu aliyewatuma.
"Toka Mei, mwaka 2023 hadi desemba mwaka jana 2024, hakuwa amelipa chochote na alikuwa anadaiwa dola 14,400 ila January 2025 amelipa kodi ya mwezi mmoja dola 800 tulijaribu kufanya suluhu naye anadai alikarabati hiyo nyumba kwa gharama ya dola 9,743 ,tulipofanya mahesabu kutoa gahama hizo hadi sasa anadaiwa dola 10800 ambazo anapaswa kulipa"Alisema wakili.
Kwa sasa Zuzan sio mpangaji wa nyumba hiyo kwani wateja wetu wanataka aondoke na tumemwandikia notice ya siku saba na tupo katika hatua ya kumtoa"
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo ila taarifa zinadai kwamba tayari jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo.
Ends...
0 Comments