PROF MBARAWA AKUBALI OMBI LA RC MAKONDA KUBORESHA RELI KANDA YA KASKAZINI

 RC MAKONDA AKUTANA NA WAZIRI MBARAWA, RELI YA KASKAZINI KUBORESHWA ILI KUIMARISHA UTALII.

By Ngilisho Tv ARUSHA 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatano Januari 08,2025 amekutana na Waziri wa Uchukuzi,  Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na kumweleza umuhimu wa KUBORESHA RELI ya Kanda ya KASKAZINI kwa ajili ya kukuza uchumi wa Taifa na mkoa wa Arusha.


 Waziri Mbarawa ameridhia ombi hilo la  Makonda la kuboresha reli ya Kaskazini (Tanga-Arusha) katika kuboresha huduma za Utalii Mkoani Arusha kwa kupunguza msongamano.

Katika mazungumzo yao,  Makonda mbali ya kusema kuwa sekta ya uchukuzi ni muhimu kwenye kukuza na kuimarisha utalii Mkoani Arusha, amesema kuboreshwa reli hiyo pamoja na kujengwa kwa bandari kavu Mkoani Arusha kutaondoa wingi wa malori ya mizigo barabarani pamoja na kusaidia katika matunzo ya barabara katika kuzisaidia kudumu muda mrefu zaidi.


Mbarawa alisema Arusha ni Mkoa muhimu kwa Utalii na uchukuzi ukiwa wa tatu kwa miruko ya ndege nchini Tanzania, akiahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Mkoa katika kufanikisha utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwemo kusimamia maboresho ya uwanja wa ndege wa Arusha, unaotarajiwa kuanza kufungwa taa hivi karibuni ambapo Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imeshatenga Bilioni 11 za kufunga taa kwenye uwanja huo wa ndege Arusha.


Ends

Post a Comment

0 Comments