By Ngilisho Tv
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili kwa mitihani iliyofanyika October/November 2024 ambapo jumla ya Wanafunzi wa Shule 680,574 kati ya 796,825 wenye matokeo ambao ni sawa na 85.41% wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV.
Akitangaza matokeo hayo leo January 04,2025 Jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed amesema “Mwaka 2023 Wanafunzi waliofaulu walikuwa 592,741 sawa na 85.31%, hivyo ufaulu umeongezeka kwa 0.10%, kati ya Wanafunzi 680,574 waliofaulu kuendelea na kidato cha tatu, Wasichana ni 367,457 sawa na 83.99% na Wavulana ni 313,117 sawa na 87.13%, hivyo Wavulana wamekuwa na ufaulu bora kuliko Wasichana”
“Wanafunzi wa kujitegemea waliofaulu upimaji na kupata sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha nne ni 4,205 sawa na 55.94%, huu ni mwaka wa kwanza kwa Wanafunzi wa kujitegemea kutahiniwa upimaji huu”
0 Comments