NAIBU WAZIRI AWAHAKIKISHIA WATAFITI WA VIMELEA VYA MAGONJWA USHIRIKIANO WA KAZI YAO

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

NAIBU Waziri ,ofisi ya Waziri mkuu Bunge ,Sera ,Uratibu ,Ummy Hamis Ndyaulanangabn ,amewahakikishia  wataalamu wa ndani na nje wa utafiti  wa vimelea vya magonjwa kwenye maabara  kwamba Serikali inatambua na kuthamini kazi nzuri wanazofanya na kuahidi ushirikiano.


Naibu Waziri ameyasema hayo,Jijini Arusha,alipokuwa akifungua Mkutano wa siku tatu wa watafiti wa Vimelea kwenye maabara, kwenye Ukumbi wa hoteli ya mount Meru,na  kusema kuwa wataalamu hao wanafanya kazi ngumu na hiyo inatokana na utayari wao .


Amesema kwamba Serikali imekuwa ikifanya uwekezaji mkubwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa maabara kuu Jijini Dar es Salaam,ambayo ni Kituo muhimu  cha kutolea mafunzo kwa wataalamu wa utafiti wa nchi za Afrika mashariki

na Serikali imewekeza maabara mbalimbali kwenye Hospitali za kibingwa ambako kuna maabara za kisasa kwa ajili ya kupima na kuchunguza vimelea  vya magonjwa mbalimbali.


Amesema  utafiti wao unahusu vimelea vya magonjwa mbalimbali hivyo ni watu muhimu kwa kuwa wanazuia vimelea vilivyopo kwenye maabara visitoke nje na kuleta athari kwa binadamu,wanyama,na mazingira.


Rais wa Chama cha wataalamu wa ulinzi na usalama wa Vimelea,( TAMSA) Dkt Zacharia Makondo,amesema ulinzi na usalama wa Vimelea ni eneo jipya la muhimu  sana  linalolenga kuwalinda wataalamu wanafanya kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo afya ya watu, Wanyama maabara pamoja na Viwandani,ambao wanaweza kuambukizwa bakteria wa magonjwa wakati wanafanya vipimo kwenye maabara.

Makondo ambae ni daktari mtafiti wa wanyama pori ,amesema Chama hicho kimesajiliwa Nchini mwaka 2020 kinashirikiana na Shirikisho la kimataifa liitwalo International Federation for Biological sefety Association ,kwa pamoja wameandaa Mkutano huo uitwao Global Voice biological biosafety & Biosecurity ,ambao ni wa siku tatu ulianza na mafunzo ya siku mbili ya kujilinda na Vimelea ,kulinda vifaa vya maabara  na Viwandani 


Wataalamu hao wa vimelea vya magonjwa ya mifugo na mimea unashirikisha watafiti 200 kutoka nchi 50 Duniani kwa ajili ya  kudhibiti ugaidi wa vimelea kulingana na utafiti wa maabara.


Ends..

Post a Comment

0 Comments