LEOPARD TOURS YAKABIDHI PIKIPIKI 20 KWA JESHI LA POLISI ARUSHA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Taasisi ya Leopard Tours imekabidhi pikipiki 20 kwa Jeshi la Poslisi Mkoani Arusha ikiwa. Ni sehemu ya kuunga Mkono juhudi za kuimarisha Ulinzi na usalama Mkoani humo, hafla fupi iliyofanyika Leo Januari 24, 2025 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Akizungumza wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Leopard Tours, Zuher Lazal amesema kuwa  hatua hiyo ya kugawa pikipiki imetokana na juhudi zilizowekwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Siluhu Hassan kwenye Sekta ya utalii ambayo inaweesha kutoa michango kwa jamii kupitia Jeshi la Poslisi.


Pia amemshukuru Mhe paul Christian Makonda ambaye amekuwa nguzo kubwa kwa kuendeleza juhudi hizo kwenye Sekta ya Utalii kwa kuzingatia kuwa Arusha ndio Kitovu cha Utalii ambapo Jeshi la Polisi ndio ndio msingi wa kuimarisha Usalama.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameishukuru Taasisi hiyo kwa uthubutu wake wa Kutoa ajira kwa vijana wa Kitanania na faida inayotokana na shughuli za utalii kurejeshwa kwa jamii kupitia kwa jeshi la polisi ili kutekeleza majukumu yao kwa wepesi.

 

“Nafasi yangu katika Mkoa huu ni Pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa kila Mwananchi wa Mkoa huu kutekeleza majukumu yake bila changamoto yoyote ikiwemo jeshi letu la Polisi”. Amesema Mhe. Makonda.


Hata hivyo amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza kasi ya kuimarisha Ulinzi na Usalama ili kuhakikisha kuwa Mkoa wa Arusha unakuwa kitovu cha Amani Duniani.












Post a Comment

0 Comments