JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO YA BILIONI 1.7 KWA AJILI YA KUTENGENEZA BARABARA ZAKE ZOTE KOROFI ,MADIWANI WACHEKELEA HAWATABURUSHWA TENA KWENYE TOPE!

Na  Joseph Ngilisho ARUSHA 

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imetekeleza mpango wake wa ununuzi wa Mtambo(Grader) na Magari Mawili yenye thamani ya sh,bilioni 1.7 kwa ajili ya matengenezo ya miundo mbinu ya barabara katika barabara zake zote korofi za jiji hilo.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa malori hayo  Mapya pamoja na Mtambo huo mpya mapema leo January 28,2025,iliyofanyika katika uwanja wa migambo jijini Arusha, Mkurugenzi wa jiji hilo,John Kayombo alisema ,kuwa nyenzo hizo zinakwenda kuondoa Changamoto katika barabara zote katika kata 25 za jiji hilo.

Aliwataka madiwani kutembea vifua mbele kwa sababu mitambo hiyo inakwenda kujibu kilio cha muda mrefu cha wananchi kwa kuondoa Changamoto ya barabara korofi.


Alisema halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha sh bilioni 2 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na malori  ila kwa neema ya mungu tu tumeweza kununua nyenzo hizo kwa thamani ya sh, bilioni 1.7 na fedha zilizobaki zitagawanywa kwa kila kata kiasi cha sh,milioni 4 kwa ajili ya ununuzi wa vifusi.


"Madiwani wangu walikuwa kwenye wakati mgumu sana waliburuzwa kwenye maji kutokana na kero ya barabara ila kwa sasa madiwani wangu tembeeni vifua mbele hakuna diwani atakaye buruzwa kwenye maji tena"

 Disemba 16 mwishoni mwa mwaka jana 2024, wananchi wa kata ya murieti waliwakamata viongozi wa kata hiyo akiwemo Diwani wa kata hiyo Francis Mbise na kuwatembeza kwenye madimbwi makubwa ya maji katikati mwa barabara zinazokatiza katika kata hiyo wakishinikiza Serikali kuwachongea barabara.


Kayombo alisema tatizo kubwa la barabara mbovu na korofi ndani ya Jiji la Arusha linaenda kumalizwa kabisa baada ya Halmashauri ya Jiji hilo kununua mitambo yake binafsi ya kuchonga barabara za mitaa yenye thamani ya bilioni 1.7.

Meya wa jiji la Arusha, Maximilian Iranghe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliishukuru halmashauri hiyo kwa kutekeleza maelekezo ya baraza la Madini kwa ununuzi wa Mtambo huo na malori na kuwataka watendaji kutumia zana hizo  kama iliyokusudiwa .


Aliwataka madiwani kwenda kuainisha maeneo korofi kwenye kata zao ili barabara hizo ziweze kutengenezwa na kuondoa Changamoto hiyo.


Awali mhandisi wa  jiji hilo ,Jacob Mwakiambiki alieleza kuwa Mitambo na Malori hayo mawili yamenunuliwa kwa fedha za ndani baada ya halmashauri hiyo kutenga kiasi cha sh, billion 2.kupitia bajeti yake ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25.


"Ndani ya mwaka huu wa fedha jiji la Arusha limefanikiwa kununua mtambo mmoja (Grader) aina ya Catapiler -Model 140GC pamoja na Malori mawili(SINOTRUK-Modl HOWO) kwa ajili ya shughulinza ukarabati na matengenezo ya barabara"


Alifafanua kwamba malori Mawili na Mtambo yamenunuliwa kwa thamani ya sh, billion 1,742,520,004.70 kwa mchanganuo kuwa gharama ya mtambo ni sh, bilioni 1,329270,000.00 na gharama za Malori mawili ni sh,milioni 413,250,004.70 ,gharama hizo ni pamoja na VAT.

 

Wakizungumzia ujio wa nyenzo hizo baadhi ya madiwani wa jiji hilo,Saluni Olodi diwani wa Sokoni one,Karimu Mushi kutoka kata ya Engutoto na Francis Mbise wa kata ya Muriet wameishukuru halmashauri hiyo kwa kuwaleta mitambo hiyo ambayo inaenda kuondoa Changamoto ya barabara ambayo ilipelekea baadhi ya madiwani kumburuzwa kwenye matope na wananchi .



Karimu Mushi diwani wa Engutoto aliishukuru halmashauri hiyo kwa kusikia kilio cha wananchi kuoitia madiwani hao na kuamua kutenga kiasi hicho cha fedha kioichofanikisha ununuzi wa mitambo hiyo.

Naye Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Arusha ,Willfred Soilel Mollel aliishukuru halmashauri hiyo kwa kutekeleza ilani ya ccm na kununua mitambo hiyo kwa ajili ya matengenezo ya barabara korofi alisema itasaidia kuwapunguzia kero wanancho hasa marabara ambazo hazipo kwenye mpango wa Tarura.


Alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa jiji kuhakikisha mitambo hiyo inatunzwa  na iwapo itaharibuka lazima mhandisi wa jiji anajiridhisha na sio kuwa mnabadilisha kifaa ili kujipatia fedha .


Aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha mitambo hiyo inaanza kazi mara moja hasa kata za pembezoni ambazo kuna changamoto kubwa ya ubovu wa barabara.







Enda..














Post a Comment

0 Comments