JAJI AMKABA KOO MSIMAMIZI WA MIRATHI ALIYEIDANGANYA MAHAKAMA,AMTAKA KULETA UPYA ORODHA YA MALI ZA MAREHEMU,JASHO LAMTOKA ALIKIMBILIA NCHINI UINGEREZA !

 Na Joseph Ngilisho-MOSHI


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Moshi,imemwamuru Msimamizi wa Mirathi ya  Mfanyabiashara maarufu nchini Moshi marehemu,Paul Kyauka Njau, aliyefariki mwaka 2002,Kuleta upya orodha ya Mali za marehemu(Inventory)baada ya kubaini kuwa hakuwahi kufunga Mirathi na mgawanyo wa mali unautata.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Msimamizi huyo wa Mirathi, Emmanuel Kyauka Njau (Ismail),hakuwa amegawa mali kwa usawa  badala yake aligawa kwa upendeleo na yeye kujinufaisha na kisha kukimbilia nchini Uingereza anakoishi hadi sasa na kuwaacha baadhi ya ndugu zake wakiwa na manung'iniko.
Baadhi ya watoto wa marehemu Kyauka wakitoka mahakamani jana!

Akitoa agizo hilo mapema leo January 30,2025 jaji Safina Semfukwe anayesikiliza shauri hilo la mirathi namba 5/2002 lililofunguliwa na baadhi ya ndugu  wakiongozwa na Catherine Kyauka wakilalamikia kutofungwa kwa mirathi ya marehemu baba yao.

Jaji alimtaka Msimamizi huyo kwenda kukaa kitako na wakili wake pamoja na ndugu zake na kuandaa upya orodha ya mali za marehemu na kuiwasilisha mara moja mahakamani .
Msimamizi wa Mirathi,Emmanuel Kyauka aliyehamia nchini Uingereza
"Haiwezekani msimamizi wa mirathi ukawa huna  nyaraka zinazoonesha orodha ya mali za marehemu ulizodai umegawa , nakuagiza kakae na ndugu zako pamoja  na wakili wako muandae hiyo Inventory na kuiwakilisha mahakamani Februali 6 ili ndugu waipitie na  kesi ianze kusikilizwa siku ya jumatatu February 10 "

Adha jaji alikataa ombi la  msimamizi huyo wa Mirathi la kutaka kuondoka na kurejea nchini Uingereza kwa madai ya kuwahi majukumu yake ya kazi ,akimtaka  kukamilisha kwanza jambo hilo la  kuorozesha  mali za marehemu kwani kesi hiyo imedumu kwa muda mrefu wa miaka 23 tangu marehemu afariki Feb,17 mwaka 2002 na akiondoka atakuwa amejikosesha haki yake ya kusikilizwa.

"Tulichobaini hapa Inventory haikuwahi kufailiwa kilichokuwa kimefailiwa hapa ni Valuation hivyo natoa oda ,kwa msimamizi wa mirathi nenda ukatuletee Inventory mpya"alisema 

Pia jaji aligoma kuahirishwa kesi hiyo na kuisogeza  hadi mwezi june mwaka huu kama alivyoiomba msimamizi wa mirathi ili aweze kujiandaa vizuri.

"Nitakuwa nachekesha kama nitaahirisha shauri hili hadi June ,mimi nafanyakazi kwa mujibu wa miongozo ya kimahakama hivyo sitaweza kufanya hivyo na kama hutakuwepo utakuwa imejikosesha haki ya msingi ya kusikilizwa"alisema Jaji.
Baadhi ya ndugu waliofika mahakamani akiwemo Richard Kyauka Njau, aliishukuru mahakama kwa uamuzi wa kumzuia msimamizi huyo wa Mirathi asiondoke nchini mpaka ahakikishe amekamikisha kuandaa orodha ya mali za marehemu kwani imekuwa vigumu sana kumpata.

"Mh Jaji tunaomba asiondoke huyu mtu ametuasumbua miaka mingi sana "Alisikika Richard akilalama mahakamani hapo!

Awali kabla ya kusikilizwa kwa shauri hilo jaji Semfukwe  aliagiza kuitwa kwa msimamizi huyo wa Mirathi aliyekuwa ugaibuni nchini Uingereza,baada ya kukosekana kwa nyaraka muhimu ikiwemo orodha ya mali za marehemu ambayo inamanufaa katika uamuzi wa shauri hilo.

Wakili wa upande wa mjibu Maombi, Daniel Ngudungi alijaribu kumshawishi jaji Semfukwe kuwa Inventory ipo kwenye nyaraka zilizopo mezani kwake ,lakini jaji alikuwa makini zaidi kwa kubaini kwamba faili lililopo mbele yake zilikuwa na nyaraka zinazoonesha uthamani wa mali(Valuation) na sio inventory inayohitajika na kumtaka mteja wake kwenda kuleta Inventory mpya ili itumike katika uendeshaji wa shauri hilo.

Naye wakili wa walalamikaji anaye mwakilisha ,Catherine Kyauka,Matuba Nyerembe alimshukuru Jaji Semfukwe kwa kubaini kwamba Msimamizi wa Mirathi, Emmanuel Kyauka hakuwahi kuleta Inventory Mahakamani ila alikaribu kuihadaa mahakama jambo ambalo jaji alibaini uongo huo.

"Maamuzi ya Jaji amemtaka msimamizi wa Mirathi kutengeneza Inventory mpya aweze kuiwasilisha mahakamani ili pande mbili ziweze kuipitia kama sheria inavyotaka na waweze kutoa maoni yao na hatimaye mirathi hiyo ya muda mrefu iweze kufungwa"

Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa February 10 mwaka huu baada ya mahakama kupokea Inventory January 6,itakayokuwa imepitiwa na pande zote.

ends ..








Post a Comment

0 Comments