Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paul Makonda amekerwa na tabia ya Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ya kuvizia ziara za viongozi wa juu kuja kutoa kero za wananchi badala ya kushiriki vikao halali vya maendeleo ambavyo amekuwa hahudhulii.
Akiongea mapema leo January 6,2025 katika ziara ya waziri wa ujenzi ,Abdallah Ulega Mkoani Arusha,ambapo mbunge Gambo alikuwepo katika mradi wa barabara ya Mianzini hadi Ngaramtoni wilayani Arumeru,yenye urefu wa Kilometa 18,Makonda alisema Gambo anaishi kwa kuvizia viongozi wa juu wanapokuja kwenye ziara ili atoe kero za wananchi lakini amekuwa hahudhulii vikao vya maendeleo. Jambo ambalo RC Makomda alisema halikubaliki na ni utovu wa nidhamu.
Katika ziara hiyo Mrisho Gambo alimtaka waziri Ulega kutoa majibu baadhi ya changamoto za miundo mbinu ikiwemo malipo ya fidia kwa wananchi wa barabara ya mita miambili upande wa jiji la Arusha katika mradi ya barabara ya Mianzini hadi Ngaramtoni.
"Hoja aliyosema Gambo hapa ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana ,kumvizia Kiongozi ili upachike Mambo Yako ,mimi spendi kumvizia Kiongozi kwenye 'public' watu wamejaa hivi unaanza kumchokekea maneno yako ,uwe unakuja kwenye kikao "
Makonda alimtaka Gambo kuacha kumchomekea Kiongozi maneno ambayo yameshajadiliwa kwenye vikao huo ni utovu wa nidhamu.
"Hatuwezi kuwa viongozi halafu unasubiri Kiongozi anakuja ,halafu ukienda pale unampachikia maneno, viongozi hawa ni watu wenye heshima,hata suala la taa za barabara lilisemwa, njoo kwenye vikao jenga hoja, usitafute umaarufu wa kijinga"
"Kwa Mfano suala la Barabara ya Kilombero tumekaa kwenye vikao vya bodi ya barabara tumeijadili na kupata kibali cha serikali barabara ile inaenda kujengwa kwa kiwango cha Lami hata kwenye kikao cha ndani na waziri jambo hili limesemwa ".
"Tunataka tuweke heshima na viongozi wetu ukihudhulia vikao utajenga hoja na tutaondoka na sauti moja, Gambo ungehudhuia vikao haya yote usinge yasema hapa serikali ya mama samia inatetea wananchi wote wanyonge "
Awali Gambo alimweleza waziri Changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo suala la Barabara ya Kilombero,aliomba barabara ziwekwe Taa ikiwemo hiyo aliyotembelea waziri ya Mianzini hadi Ngaramtoni na kumtaka waziri atoe tamko juu ya malipo ya fidia kwa wananchi
Ends..
0 Comments