GAMBO AIBUKA NA KUMWAGA MBOGA ,ALIPONZWA NA KAMDOMO RC AKAMSHUGHULIKIA 'PERPENDICULAR'

Na Joseph Ngilisho,ARUSHA

SAKATA la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, dhidi ya Mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo limechukua sura mpya mara baada ya Makonda kuamua kumkemea hadharani mbunge huyo akidai  ni mtovu wa nidhamu anayesaka umaarufu wa kijinga.

Hata hivyo Gambo ameibuka na kujibu mapigo  kuwa hakuna mtu yeyote wa kumtisha na kumzuia kuwasemea wananchi wake kwa Kiongozi yoyote wa serikali na alimtuhumu RC Makonda kuwa hajui sheria na taratibu za Mbunge kushiriki vikao mbalimbali na kutaka mkuu huyo wa mkoa aelimishwe wajibu wa  mbunge.


Gambo alisema kuwa yeye kama mbunge anawajibu wa kuwasemea wananchi Wake muda wowote na kwa wakati wowote atakapokutana na waziri yoyote mwenye dhamana.


Gambo alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa yeye hajatokea  chama cha Mapinduzi bali alitokana na Chama cha Mapinduzi .

Makonda akiwa na waziri wa ujenzi ,Abdallah Ulega Mkoani Arusha, kwenye ziara ya kutembelea mradi wa barabara ya Mianzini hadi Ngaramtoni wilayani Arumeru,yenye urefu wa Kilometa 18,Makonda alisema Gambo anaishi kwa kuvizia viongozi wa juu wanapokuja kwenye ziara ili atoe kero za wananchi lakini amekuwa hahudhulii vikao vya maendeleo. Jambo ambalo RC Makomda alisema halikubaliki  na ni utovu wa nidhamu.


Katika ziara hiyo Mrisho Gambo alimtaka waziri Ulega kutoa majibu baadhi ya changamoto za miundo mbinu ikiwemo malipo ya fidia kwa wananchi wa barabara ya mita miambili upande wa jiji la Arusha katika mradi ya barabara ya Mianzini hadi Ngaramtoni.




"Hoja  aliyosema Gambo hapa  ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana ,kumvizia Kiongozi ili  upachike Mambo Yako ,mimi spendi kumvizia Kiongozi kwenye 'public' watu wamejaa hivi unaanza kumchokekea maneno yako ,uwe unakuja kwenye kikao "



Makonda alimtaka Gambo kuacha kumchomekea Kiongozi maneno ambayo yameshajadiliwa kwenye  vikao huo ni utovu wa nidhamu.




"Hatuwezi kuwa viongozi halafu unasubiri Kiongozi anakuja ,halafu ukienda pale unampachikia maneno, viongozi hawa ni watu wenye heshima,hata suala la taa za barabara lilisemwa, njoo kwenye vikao jenga hoja, usitafute umaarufu wa kijinga"



"Kwa Mfano suala la Barabara ya Kilombero tumekaa kwenye vikao vya bodi ya barabara tumeijadili na kupata kibali cha serikali barabara ile inaenda kujengwa kwa kiwango cha Lami hata kwenye kikao cha ndani na waziri jambo hili limesemwa ".



"Tunataka tuweke heshima na viongozi wetu ukihudhulia vikao utajenga hoja na tutaondoka na sauti moja, Gambo ungehudhuia vikao haya yote usinge yasema hapa serikali ya mama samia inatetea wananchi wote wanyonge "


Awali  Gambo alimweleza waziri Changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo suala la Barabara ya Kilombero,aliomba barabara ziwekwe Taa ikiwemo hiyo aliyotembelea waziri ya Mianzini hadi Ngaramtoni na kumtaka waziri atoe tamko juu ya malipo ya fidia kwa wananchi  




Ends..


Post a Comment

0 Comments