DR SLAA AFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUSOMEWA SHTAKA MOJA

By Ngilisho Tv 

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Wilbroad Slaa (76) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo January 10,2025 jijini Dar es Salaam, kujibu shtaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa X (zamani Twitter).


Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la kila siku la Mwananchi, mapema leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kumshikilia Dk. Slaa.


"Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye," amesema Kamanda Muliro.


Taarifa ya kukamatwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kukamatwa na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni, Dar es Salaam.


Dkt. Slaa aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchi Sweden kuanzia Novemba 2017, baada ya kuteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli, kabla Rais Samia Suluhu Hassan kumvua wadhifa huo mwaka 2023.


Pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema kabla ya kujiondoa katika chama hicho mwaka 2015.

Post a Comment

0 Comments