DKT MPANGO ATAKA KUIBULIWA TAARIFA ZA UKATILI KWA JAMII

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Watanzania wote kuibua taarifa zinazohusu vitendo vya ukatili ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.


Makamu wa Rais ametoa wito huo alipomwakilisha Rais  Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya

Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) yaliyofanyika katika

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.


Amesema wapo wanawake, watoto na wanaume wanaopitia vitendo vya ukatili wa

kijinsia au kimwili lakini hawatoi taarifa kwenye vyombo vya sheria, vilevile baadhi ya

mila na desturi zimekuwa zikitumika kuwakandamiza waathirika.


Amesema pamoja na dhamira njema ya Serikali ya kuhakikisha usawa wa kijinsia

hapa nchini, bado wanawake ambao idadi yao ni zaidi ya nusu ya watu hapa nchini,

wanapewa nafasi ndogo katika umiliki wa mali na wanabaguliwa kwa msingi wa

jinsia.


Ameongeza kwamba kwa mujibu wa Mpango wa Kitaifa wa Kupinga vitendo

vya Kikatili dhidi ya Wanawake wa mwaka 2016, kati ya wanawake kumi, 4

wamepitia ukatili wa kimwili, na mmoja kati ya watano wamepitia ukatili wa kingono

miongoni mwao wakiwa na umri mdogo (chini ya miaka 15).


Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema kulingana na Ripoti ya UN Women Social

Institution and Gender Index (SIGI) 2022, ukatili wa kijinsia nchini Tanzania

unabainishwa zaidi kupitia ndoa za utotoni, ubaguzi ndani ya familia, ukatili dhidi ya

wanawake, ukosefu wa uhuru katika kupanga uzazi, upatikanaji na umiliki wa ardhi.


Pia kulingana na Taarifa ya Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania iliyoandaliwa na

Benki ya Dunia mwaka 2022, 40% ya wanawake wote wenye umri wa miaka 15 hadi

49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili na 17% wamepitia ukatili wa kingono.


Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

imejizatiti kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake hapa nchini

kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo

inasimamia masuala ya usawa wa kijinsia.


Amesema dhamira hiyo ya Serikali

inaonekana zaidi kupitia mikakati, mipango na sera za kitaifa kama vile Dira ya

Maendeleo ya Taifa 2025, Mipango ya Maendeleo ya Taifa ya Miaka Mitano, Mkakati

wa Kitaifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (NSGR) na Sera ya

Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya 2000.


Ameongeza kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt.

Samia Suluhu Hassan, imedhihirisha kwa vitendo dhamira yake ya kuboresha

utendaji katika utoaji haki, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usawa wa kijinsia katika

ngazi mbalimbali za uongozi wa Mahakama ambapo kwa takwimu, Mahakama ya

Rufani, 33% ya Majaji ni wanawake, Mahakama Kuu, ni 38%.


Kwa Wasajili wa Mahakama ,wanawake ni 33% na Naibu wasajili ni 48.72%. Aidha, wanawake ni

50% ya Mahakimu wa Mahakama za Mahakimu Wakazi na 41% ya Mahakimu wa

Mahakama za mwanzo.


Makamu wa Rais ametoa wito wa kujenga tabia ya kutambua na kusheherekea

mafanikio ya wanawake katika jamii ili kutoa hamasa kwa wasichana na wanawake

wengine kujifunza na kuiga mifano hiyo.


Amesema ipo mifano ya wanawake hapa

nchini waliofanya vizuri katika fani mbalimbali kwa kuanza na Rais Mheshimiwa Dkt.

Samia Suluhu Hassan, Rais wa kwanza mwanamke; Bibi Titi Mohamed, mwanamke

aliyekuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa nchi pamoja na wengine

wengi.


Aidha amesisitiza umuhimu wa Majaji na Mahakimu wanawake nchini walioko katika

utumishi na waliostaafu, kuhakikisha wanajiunga au wanahuisha uanachama wao wa

TAWJA kwa kulipa ada. Amesema TAWJA inahitaji mshikamano na ushiriki wa

wanachama wake wote ili kufikia malengo yake.


Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa dhamira njema na kuendelea

kuiwezesha Mahakama ambapo Majaji wa Mahakama ya Rufani wameongezeka

kutoka Majaji 17 mwaka 2021 hadi Majaji 40 mwaka 2025.


Mhe. Prof Juma amesema ni jukumu la Majaji na Mahakimu kuitumia Dira ya

Maendeleo ya Taifa 2050 ili kufikia malengo yaliyotajwa ikiwemo vipengele vyote

vinavyotaja masuala ya kijinsia na kisheria.


Awali akitoa taarifa, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake

Tanzania (TAWJA) Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel amesema

mafaniko yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 25 ya TAWJA yanatokana na

mifumo imara ya usawa kijinsia hapa nchini pamoja na ushirikiano mzuri kutoka

katika Serikali na Mahakama ya Jamhuri ya Tanzania na Mahakama ya Zanzibar.


Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) kilianzishwa mwaka

2000 ambapo kinasherehekea Jubilei ya miaka 25 yenye kauli mbiu isemayo “Jubilei

ya Miaka 25 ya TAWJA: Kusherehekea Utofauti na Mshikamano katika Usawa wa Kijinsia”

Ends..


Post a Comment

0 Comments