Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Chama cha mapinduzi (CCM) kimempigia magoti Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia kibarua kingine aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa.
CCM wametoa Ombi hilo leo January 29,2025 wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati Mtahengerwa na Mkuu mpya wa Wilaya hiyo,Joseph Mkude aliyeteuliwa akitokea Wilaya ya Kishapu.
Mtahengerwa aliyehudumu katika Ofisi ya Ukuu wa Wilaya ya Arusha kwa miaka miwili pekee tangu January 25,2023 alipoteuliwa, ameondoka rasmi katika nafasi yake January 24,2025 baada ya kutenguliwa na Rais Samia.
Akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Willfred Soilel Mollel alisema kuwa uamuzi wa Rais Samia kumtengua mkuu huyo wa Wilaya hawawezi kubishaniwa lakini wanachoweza ni kumuomba ampe kibarua kingine kutokana na imani kubwa waliyonaye kwa Kiongozi huyo.
"Utenguzi huu sisi hatuna la kusema, kwa sababu aliyetekekeza ni Rais aliyemuweka madarakani ambaye hatuwezi kuhoji kwa hilo, ila tunachoweza ni kumuomba ampe Felician (Mtahengerwa )kibarua kingine kwani Bado ni kijana na ana nguvu anaweza kufanya kazi Bado" alisema Soilel.
Naye Mtahengerwa amesema kuwa anawashukuru watumishi wenzake kwa ushirikiano alioupata kwa mda wote aliofanya kazi katika nafasi yake ya Ukuu wa Wilaya na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa namna nyingine katika kujenga taifa.
Kwa upande wake DC,Mkude ambaye amepokea kijiti hicho alimshukuru rais Samia kwa kuendelea kumwamini na kuahidi kutomwangusha kwa utumishi uliotukuka.
Aliahukuru jwa mapokezi mazuri ya watumishi wenzake na kuomba ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.
"Mimi ndio kwanza mgeni, Sina ninachojua hivyo ninapomkimbilia yoyote kati yenu kuomba msaada wa jambo naombeni ushirikiano kuhakikisha wilaya yetu inafanikisha malengo yake ya hasa miradi ya maendeleo na utatuzi wa kero za wananchi" amesema.
ends
0 Comments