Assumpter aahidi kuendeleza ushirikiano katika kutoa elimu kwa vikundi vya fedha (Vicoba) ili kuvinufaisha zaidi
Na Lydia Lugakila
Bukoba.
Kauli hiyo imetolewa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge mhe. Assumpter Mshama alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kagera hivi karibuni katika uzinduzi wa siku ya Ijuka Omuka
Aliwahimiza Watunza fedha za vikundi Mkoani humo wakiwemo Wana Misenyi juu ya kuwa waaminifu katika masuala ya fedha ili kunufaika zaidi badala ya kujutia walichowekeza huku akitaka akina mama wapate furaha na fedha zao na sio majonzi.
Bi, Assumpter amesema kuwa baadhi ya Wananchi wamekuwa wakijinyima kwa kuchanga fedha kupitia vikundi mbali mbali hivyo watunza fedha wanatakiwa kuwa waaminifu ili kila mmoja apate alichowekeza baada ya kufikia wakati wa kugawana
Aidha Bi Assumpter amesema kuwa ataendelea kuwapatia ushirikiano wa kutosha na yupo tayari kuendelea kutoa elimu kuhusu vikundi hivyo (Vicoba) ili kila mtu anufaike kadili anavyokuwa amewekeza.
Ikumbukwe kuwa Mhe. Assumpter alikuja na kauli mbiu ya "Umaskini sio fungu langu" wakati akiomba ridhaa ya kuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge huku akihamasisha Wananchi wa Jimbo la Nkenge hasa wanawake kuwekeza pesa (Vicoba) kwa ajili ya maendeleo yao binafsi.
0 Comments