ZIWA DULUTI LINAVYONOGESHA MAPATO TFS,WATALII WA NDANI WAONGEZEKA MLIMA WA MAOMBI WAWA KIVUTIO!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

                    

WAKALA wa Misitu Tanzania (TFS)imeanza kutangaza vivutio vyake vya utalii ndani ya misitu ikiwemo utalii wa Ziwa Duluti na kuwaita wageni  kutoka ndani na nje ya nchi kuja kujionea mandhari nzuri ya utalii wa mazingira asilia ya ziwa hilo lenye mlima wa Maombi.

Hayo yamesemwa  wilayani Arumeru na Ofisa Misitu, Anna Lawuo wakati alipozungumzia ujio wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika (AAAG) waliotembelea ziwa hilo kujionea vivutio vya utalii vya misitu iliyopandishwa hadhi huku maeneo yanayotekelezwa katika shughuli za utalii yakiwa ni 33 ikiwemo yale yaliyopo ndani ya mashamba ya misitu.


Alisema misitu hiyo imepandishwa hadhi kuwa misitu ya mazingira asilia sababu ni maeneo yenye viumbe adimu visivyopatikana ulimwenguni kote ikiwemo misitu yenye miti adimu yenye wanyama na wadudu wote.


“Tunafanya utalii ulikolojia ikiwemo utafiti na mafunzo na kwa hapa Ziwa Duluti ni sehemu iliyohifadhiwa misitu na ni maarufu kwaajili ya maombi na kufanya utalii wa kutembea msituni, maombi na kutembea ziwani.


Alisema ziwa hilo ni maarufu sana katika kufanya maombi, utalii wa maji , uvuaji samaki na utalii wa maji kwa kutumia makasia ya asilia  lakini pia utalii huu hupelekea utulivu wa akili na mwili”


Alisisitiza wageni kutoka ndani na nje wanakaribishwa kutembelea eneo hilo la Duluti na maeneo mengine ya TFS kwa ajili ya kusikia milio ya ndege, utulivu wa akili, kutembea ziwani alitoa rai nyakati hizi za sikukuu kutembelea hifadhi za TFS ili kujione vivutio hivyo.


Naye Mhifadhi  Mwandamizi wa Misitu Wilayani Arumeru, kutoka TFS , Peter Myonga amesema katika hifadhi hiyo wanafanya shughuli za uhifadhi mazingira ikiwemo kusimamia shughuli za  utalii kwakushirikiana na wananchi.

Alisema kiasi cha shilingi milioni 400 zimekusanywa katika Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Ziwa Duluti ikiwa ni mapato yaliyotokana na wageni wa ndani na nje kwenda kutalii katika Ziwa hilo lililopo Mkoani Arusha.

Alisema mapato ya serikali katika Msitu wa Ziwa Duluti yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka kutokana na watalii wengi wa ndani na nje kwenda kutalii katika Ziwa Duluti na kujionea vivutio mbalimbali adimu vilivyoko katika Msitu huo.


Myonga alisema mwaka mwaka wa fedha julai 2022/23 watalii wa ndani 16,760 walitembelea Ziwa Duluti ikiwa ni pamoja na watalii wa nje 6,700 na shilingi milioni 46 zilikusanywa kama mapato ya serikali.


Alisema katika kipindi cha mwaka 2023/24 jumla ya shilingi milioni 106 zilikusanywa ikiwa ni mapato ya wageni kutoka ndani ya nchi na nje na kuvuka malengo ya mwaka uliopita.


Mhifadhi huyo Mkuu alisema kuwa katika muda mfupi wa miezi mitano cha kuanzia julai 2024/25 hadi novemba mwaka huu watalii wa ndani waliokwenda kutembelea Ziwa Duluti ni watalii 8,680 na wageni kutoka nje ya nchi watalii 7000 na mapato ya serikali milioni 70 yamekusanywa hiyo ni miezi minne tu kiasi hicho kimekusanywa na huenda hadi kufika june mwakani makusanyo yanaweza kuvuka malengo zaidi.


Myonga alisema kuwa Utalii uliopo katika Msitu wa Hifadhi ya Ziwa Duluti ni pamoja na utalii wa Majini,Utalii wa Msitu,Utalii wa Uvuvi wa Samaki,Utalii wa Picha,Utalii wa Utafiti,Utalii wa kutembea bila viatu{pekupeku} na Utalii wa maombi.


Alisema watalii wengi wa ndani wanakwenda kutalii katika Msitu wa Ziwa Duluti kwa ajili ya utalii Utalii wa Maombi hususani siku za wiki za mapumziko kazi kwani mamia ya watanzania huenda katika Hifadhi hiyo kutalii Utalii wa Maombi na kuingizia serikali mapato.


Mhifadhi Mkuu Myonga alisema mbali ya Utalii wa Maombi na vivutio vingine ambavyo kwa pamoja vimewapa ajira vijana zaidi ya 200 kwa kununuwa mitumbwi na kutembezwa katika ziwa Duluti na kuwa na uhakika wa kipato kwa siku.



                               






Ends..


Post a Comment

0 Comments