Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MKURUGENZI wa Hospital ya Selian iliyopo Ngaramtoni wilayani Arumeru Mkoa wa ARUSHA,Amon Marti ameingia matatani akituhumiwa kuwanyanyasa kingono, kipigo na matusi wafanyakazi wake wa kike ikiwemo kumshushia kipigo mtumishi wa Hospital hiyo pamoja na kumtimua kazi bila kufuata taratibu baada ya kumkatalia takwa la kingono.
Kufuatia tuhuma hizo waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mkoani hapa,inayomiliki kanisa hilo la KKKT,wameibuka na kutaka Mkurugenzi huyo aondolewe madarakani kwani amekuwa sugu kwa matukio ya kujirudia bila kuchukuliwa hatua zozote na analitia aibu kanisa hivyo wametishia kuandamana iwapo askofu wa kanisa hilo , Godson Abel Mollel ataendelea kumkumbatia bila kuchukua hatua stahiki dhidi yake.
Wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya waumini hao ,Mathias Lyimo na Isaac Lukumay walimwomba askofu wao,Godson Mollel kumchukulia hatua Mkurugenzi huyo kwani mbali na kuwadhalilisha wafanyakazi ,amelidoa kanisa katika miradi yake.
"Kuna wakati tume iliundwa ya uchunguzi wa matukio ya Mkurugenzi huyo na kubainika kuwa anahusika lakini hakuna hatua zozote zimechukuliwa tunaochiomba askofu amwondoe kabla hatujaitisha maandamano ya kumpinga askofu kwa kumlea mhalifu"
Mmoja ya watumishi wa hospitali hiyo,(jina linahifadhiwa)anayefanyakazi kitengo cha uangalizi wa watoto wenye ulemavu, OCCUPATIONAL THERAPY (REHABILITATION) alidai kunyanyaswa kingono na mkurugenzi huyo na Kisha kumshushia kipigo na baadaye kumfungia stoo ya vifaa tiba kabla ya kuokolewa na polisi na baadaye kutimuliwa kazi.
Alisema chanzo cha yeye kufanyiwa ukatili huo ni baada ya kutoa taarifa kwa mfadhili juu ya tukio la vifo vya watoto wawili ambao ni miongoni mwa watoto wenye ulemavu wanaopatiwa huduma bure katika hospitali hiyo chini ya Mradi wa mfadhili huyo,ambapo Mkurugenzi hiyo hakutaka taarifa za vifo kuelezwa Mfadhili ili aendelee kuleta fedha anazotoa kulingana na idadi ya watoto wanaohudumiwa hapo.
"Chanzo cha Mkurugenzi wangu kunichukia ni suala la mimi kumkatalia takwa lake la kimapenzi ,pia tukio la juzi la kutoa taarifa kwa Mfadhili kuhusu vifo vya watoto ndo limemkasirisha zaidi kwani hakutaka nitoe taarifa hiyo ili aendelee kupokea fedha za marehemu jambo ambalo kama mimi mkuu wa kitengo nisinge weza kukaa kimya"Alisema
Alisema mkurugenzi alichukizwa na hatua ya mtumishi huyo kutoa taarifa baada ya mfadhili kutembelea idara yake na kutaka kujua maendeleo ya watoto.
"Ilikuwa siku ya jumatatu wiki hii mkurugenzi alitangaza kunihitaji ofisini kwake ,nilienda katika kikao hicho na kukuta watu wengi sana alinihoji kwa ukali kwanini nimetoa taarifa ya vifo vya watoto kwa mfadhili,unataka mfadhili aondoke fedha zitapatikana wapi"??Alihoji
"Mkurugenzi huyo aliagiza niandikiwe barua ya kufukuzwa kazi na kunitaka niondoke katika kikao hicho ,nikiondoka na kwenda ofisini kwangu na kuendelea na shughuli zangu wiki iliyofuata alinifuata ofisini na kunitukana sana na baadaye alianza kunipiga makofi na Kisha alinifungia ndani na kuondoka na funguo"
"Nikiwa peke yangu ofisini nimefungiwa nilichukua simu yangu na kuwapigia polisi kuomba msaada na polisi walipofika ,aliagiza nifunguliwe na nikabidhiwe barua ya kufukuzwa kazi niondoke na nisionekane Tena hapo"
"Ni heri niseme ukweli kuliko kukaa kimya waendelee kula fedha za marehemu ,unajua huyu mfadhili huwa anakuja na kutaka taarifa za maendeleo ya watoto na Mimi kama mkuu qa idara nampatia taarifa "
Alisema kabla ya tukio hilo Mkurugenzi Dkt Mart alikuwa alinifuata ofisini mtumishi huyo na kumshikashika maziwa alimtaka kimapenzi ofisini huku alimwambia 'ukitaka hayo mambo yaishe kubali tumalize hapa hapa'
Alisema Dkt Marti alishawahi kumwandikia barua ya kumfukuza kazi kabla ya wafanyakazi wenzake kulalamika na kutishia kumshtaki ndipo alipoagiza arejeshe kazini baada ya kukaa nje ya kazi miezi minne.
Mtumishi huyo ambaye amefanyakazi Selian kwa zaidi ya miaka 15, ameiomba serikali kuingilia kati ili aweze kupata haki zake kwani wafanyakazi wanateseka sana na wameshangaa kuona mkurugenzi akifanya vituko kwa watumishi wake bila kuchukukiwa hatua yoyote na wamiliki wa hospitali hiyo ambao ni kanisa la KKKT.
Aidha alisema kuwa baada ya kudhalikishwa na kufikiwa ofisini na kupigwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi Usa River wilayani humo na mtuhumiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na baadaye kupata dhamana.
Hata hivyo alisema polisi wanaendelea na upelelezi wa suala hilo ili kumfikisha mtuhumiwa Mahakamani.
Kwa upande wake askofu wa Kanisa hilo ask Godson Abel Mollel alipohojiwa juu ya tuhuma za Mkurugenzi huyo alijibu kuwa masuala yote yanayohusu kanisa hilo yanaahughulikiwa na dayosisi bila kufafanua kama analijua tukio hilo.
Alipoulizwa juu ya malalamiko ya waumini wa kanisa hilo kuhusu Mkurugenzi huyo wa hospitali alisema hajapata taarifa na kumtaka mwandishi awashauri waumini hao kufikisha kilio chao ofisini kwake.
"Kwanini usiwashauri hao waumini waje ofisini. Kwangu maana kanisa linataratibu zake za kiutendaji"alisema askofu
Akihojiwa kwa njia ya simu dkt Amoni Marti alikana kumfahamu mtumishi huyo na kusema KUWA hakuna mtu aliyepigwa na kufukuzwa kazi katika hospitali hiyo.
"Mimi huyo mtu simfahamu nafikiri ni vizuri umhoji vizuri yeye mwenyewe na hapa hospitalini hakuna shida yoyote na hakuna mfanyakazi wa namna hiyo Selian"Alisema Dkt Mart na Kukata simu bila kufafanua zaidi.
ends....
0 Comments