WATU 179 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE YA ABIRIA BAADA YA KUANGUKA

 Watu 179 wamefariki dunia baada ya ndege ya abiria kuanguka nchini Korea Kusini.

By Ngilisho Tv 

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800, iliyokuwa ikimilikiwa na shirika la ndege la Jeju Air, ilikuwa imebeba abiria 181 na ilikuwa ikitokea Bangkok, Thailand, kuelekea Uwanja wa Ndege wa Muan.


Picha mbalimbali za video zinaonesha ndege hiyo ilipokuwa ikitua na kuteleza nje ya njia ya kutua, kugonga ukuta, na kulipuka moto. 


Sababu ya ajali haijathibitishwa rasmi, lakini huduma za zima moto zinasema inaweza kuwa ilisababishwa na ndege kugongana na ndege wengine (bird strikes) na hali mbaya ya hewa.


Watu wawili waliopatikana wakiwa hai ni wafanyakazi wa ndege hiyo. 

Kila Nafsi itaonja Umauti. 




Credit 

BBC News

Post a Comment

0 Comments