WARAHIBU DAWA ZA KULEVYA KICHEKO ,POLISI YAWAMWAGIA MAPESA YA MITAJI WASIMULIA WALIVYOKABA WATU NA KUPORA!

 Na. Joseph Ngilisho,ARUSHA 



Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha katika kilele cha Siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoani humo wametoa mitaji  kwa warahibu wa dawa za kulevya ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.


Akiongea wakati wa kukabidhi mitaji hiyo katika maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili na utumiaji wa dawa za kulevya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi amebainisha kuwa baada ya serikali kutoa huduma ya tiba kwa warahibu hao, wameona ni vyema kuunga juhudi hizo kwa kutoa mitaji ya biashara ili  iweze kuwaingizia kipato,  kuwakwamua kiuchumi na  pia kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.


Aidha SSP Matagi ameitaja baadhi ya misaada waliyoitoa kwa vikundi vya warahibu hao ni vifaa vya saluni ya kike na kulipia kodi ya pango ya saluni hiyo kwa muda wa miezi sita.


Alifafanua kuwa jumla ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya mitaji  ni kiasi cha  sh, mil. 4,580,000 ,ambapo kiasi cha sh, 500,000 ni kwa ajili ya biashara ya matunda na mbogamboga, sh, 500,000/= kwa ajili ya utengenezaji wa sabuni, na Sh, 500,000 kwa ajili ya biashara ya mtumba.


Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Afya ya akili katika Hospitali hiyo ya Rufaa Mount Meru Dkt. Salum Seif alisema kituo hicho kilianza na jumla ya warahibu 12 ambapo mpaka sasa kinahudumia warahibu 746 ambapo wameona ni vyema kupitia siku 16 za kupinga ukatili kuwashirikisha wadau ikiwemo Jeshi la Polisi ili kulifikia kundi hilo ambalo ni wahanga wa ukatili wa kisaikolojia na uchumi.


Akimwakilisha mganga mfawidhi wa hosipitali hiyo ,Angel Kimati amewapongeza warahibu wa dawa za kulevya kwa uamuzi wao wa  kufika katika kituo hicho na kupewa tiba huku akiwataka kutumia vyema mitaji waliyoipata Kwenda kukuza vipato vyao  lakini pia kujikwamu kiuchumi na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuwasaidia wakati wote.


Mmoja ya wanufaika wa mitaji hiyo , Ratifa Abdi mbali na kulishukuru Jeshi la Polisi, alisema vitendea kazi na mitaji waliyopatiwa itawasaidia kuwaongezea vipato na Kwenda kuwa msaada mkubwa katika familia zao lakini pia kuwaepusha  na matumizi ya dawa za kulevya.


Baadhi ya warahibu wanaopata huduma ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya katika hospital hiyo,Ibrahim Mohamed na Self Omari Mkazi wa Usa River,walishukuru huduma wanayopatiwa ya kuachana na matumizinya dawa za kulevya.

Omari alisema kabla ya kuokolewa na matumizi ya dawa za kukevya baada ya kuwa mwasilika kwa miaka 11 ,alisema alikuwa na hali mbaya kiasi cha kujiingiza kwenye uporaji na kunusurika kuuawa na wananchi kwa kipigo.





Ends...




Post a Comment

0 Comments