TAZAMA PICHA 15 ZA NGUVU MAOMBI YA RC MAKONDA ARUSHA ,AOMBEWA AELEZA MAGUMU ALIYOPITIA BAADA YA KUKOSA KAZI ,AAMUA KUTUPA MSHAHARA WAKE WOTE MADHABAHUNI!,ATAKA ARUSHA UWE MKOA WA MAOMBI!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

MAELFU ya Wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi kushiriki mandamano ya maombi  maalumu ya kuombea amani huku Mkuu wa Mkoa RC Paul Makonda akitangaza Arusha uwe mkoa wa Maombi .


Maombi hayo ambayo yalianzia mzunguko wa mnara wa saa (clock Tower)  yakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Dini zote mkoani hapa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Paul Christian Makonda,viongozi hao wa dini walitilia mkazo suala la kuilinda amani yetu kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake.



Maombi hayo ambayo yaliandaliwa na Rc Makonda ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sherehe za miaka 63 ya Uhuru, yenye kauli Mbiu "Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara; Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu"yalilenga kuliombea taifa pamoja na viongozi wake kuendelea kuidumisha amani iliyoasisiwa na watangulizi wa nchi hii.



Katika viwanja vya msikiti wa ijumaa ambako maandamanonya maombi yalihitinishwa ,Mkuu wa Mkoa Paul Makonda aliwataka viongozi wa dini kuandaa matamasha ya maombi na mihadhara ambayo yeye atagharamia lengo ni kuhakikisha jamii inaokoka na kumrejea mungu.


"Lazima tuwe na siku ya kumtafakari mungu ,tunataka watu wamwabudu mungu,viongozi wa dini waandae Makongamano ya maombi ya kumwabudu mungu na mimi niambieni jitagharamia,watu wa Arusha hakuna kuchukulianmzaha auala la Maombi"Alisema.


RC Makonda alienda mbali zaidi kwa kueleza namna  alivyopitia magumu kipindi hana kazi miaka 3 na miezi 6 ikiwemo kushitakiwa mahakamani,kudhihakiwa na kukimbiawa na Marafiki.


Alisema baada ya kupata kazi kuwa  katibu wa itikadi na uenezi( ccm)Taifa ,aliamua kumshukuru mungu kwa kutotumia malipo yake ya mshahara badala yake fedha zote alipeleka Madhabahuni.

"Tangu nimepata kazi ya uenezi wa CCM na sasa Mkuu wa Mkoa sijawahi kula mshahara wangu nimekuwa nikipeleka Madhabahuni"

Katika hatua nyingine Makonda alilipongeza kabila la wachaga kwa kuwa na utamaduni wa kila mwishoni mwa mwaka kurejea nyumbani kwao akidai utamaduni huo unapaswa kuigwa na makabila mengine kwani haulengi kuheshabiwa kama wanavyosema watu bali ni kukutana na kujadili masuala ya  maendeleo na changamoto na mafanikio.


Mkuu huyo wa mkoa awaliwataka wanafamilia wote mkoani hapa kutumi,a siku ya Desemba 24 kukaa kikao cha Familia na kijadili masuala mbalimbali ya maendeleo.


Maombi hayo ambayo yalivamiwa na mvua kubwa baadhi ya viongozi wa dini wakiongizwa na Askofu Israel Maasa walimwombea RC Makonda pamoja na Rais Samia.














       




Ends..


Post a Comment

0 Comments