Tamasha kubwa la Garuka Consert kunguruma Desemba 23 Kagera, Mc Mtawala aja kivingine
Na Lydia Lugakila
Bukoba
Tamasha kubwa na la aina yake lijulikanalo kama Garuka Consert lenye maana ya kuwakumbusha wazawa wa Mkoa wa Kagera kurudi nyumbani linatarajiwa kunguruma katika mji wa Bukoba Mkoani Kagera Mnamo Desemba 23, 2024 huku mila na desturi pamoja na tamaduni za kihaya zikienziwa kupitia mziki wa asili utakaopambwa na wasanii wa Mkoa huo pamoja na uzinduzi wa Albam ya YOO MAWE iliyobeba nyimbo 16 kutoka kwa Mc Mtawala.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari katika ukumbi wa prince hotel uliopo Manispaa ya Bukoba msemaji wa Tamasha la Garuka Consert Edigar Mtawala amesema kuwa tamasha hilo ambalo litaambatana na uzinduzi wa Albam ya YOO MAWE ni safari ya kwanza ki mziki kwa msanii wa nyimbo za kiafrika Dkt Edson Mtawala maarufu Mc Mtawala.
Edigar alisema kuwa tamasha hilo litafanyika katika maeneo ya Eco beach Bukoba, ambapo wasanii mbali mbali wa Mkoa huo watatumbuiza kwa nyimbo za asili huku akieleza maandalizi kuelekea tamasha hilo kuendelea vizuri ambapo pia aliwahimiza wakazi wa Mkoa huo walioko ndani na nje ya Nchi kujitokeza kwa wingi kujionea tukio hilo la kihistoria.
"Tamasha hili limebeba mizinga 16 ambayo itasikika katika spika za Eco Beach hiyo ni heshima kwa safari ya kwanza ya kurudi nyumbani na nyumbani ni nyumbani na mgeni rasmi ni Profesa Anna Tibaijuka alisema Mc Mtawala.
Aliongeza kuwa tukio hilo litaweka heshima nyumbani Kagera huku akiwakumbusha wana Bukoba kujumuika Desemba 23,2024 kuanzia majira ya saa kumi jioni ili kufahamu mengi ya asili ya Mkoa huo huku akiahidi zawadi ya Albam bure kwa watakaojitokeza kwa wingi.
"Nia na madhumuni ni Wana Kagera kupata mziki wa asili na tutafanya hivi kila Desemba na kwa Wilaya ya Muleba, Karagwe Mwanza na Wilaya nyingine zatafikiwa ikiwemo Mkoa wa Dar es salaam na katika nyimbo hizo nimemtumia lugha mbali ikiwemo kiswahili ikiwa ni heshima kwa Mhe. Rais Samia"alisema Msanii huyo.
Aliongeza kuwa ametumia lugha ya Kiganda,Kinyarwanda katika nyimbo zake kutokana na mshikamano uliopo Kati ya Nchi hizo jirani na kuwa tamasha hilo kwa miaka ijayo anatamani lifanyike Nchi zote na kuwa kwa mwaka 2025 anataraji Tamasha la pili litakuwa kubwa zaidi.
Aidha aliwataka Vijana waliopo katika sanaa kutokata tamaa bali wajikite kufanye sanaa yenye ubunifu na kulitazama soko la kidunia pamoja na kutazama fursa ulimwengu na kuachana na Biashara ya kimazoea ikiwemo kujuana juana kwa mtu kwani hali hiyo itawaumiza na kuwaangusha hivyo wahakikishe wanapambana ipasavyo.
Naye mwimbaji wa mziki wa asili na mchekeshaji Theonest Rwegelela maarufu Omugurusi wa kanazi ameahidi kufanya makubwa katika tamasha hilo la Garuka Consert huku akilenga zaidi Vijana wa Mkoa huo na waishio nje ya Mkoa wa Kagera kuijua asili yao mila tamaduni pamoja na kukumbuka nyumbani kwao ambapo pia aliwaomba wazee wa busara maarufu wagurusi ambalo ni neno la kihaya kuwa na busara ikiwa ni pamoja na kuwafundisha maadili watoto.
Hata hivyo kwa upande wake Mwimbaji wa mziki wa asili Kagera Martin Jasson (Mart mstaarabu) ambaye ana miaka 13 katika Sanaa amempongeza Mc Mtawala kwa kuandaa tamasha hilo huku akiahidi kufanya jambo kubwa Mnamo Desemba 23 Mwaka huu ambapo pia alitamani matamasha ya aina hiyo kuwepo walau kila mara ili kuwainua wasanii hao.
0 Comments