STEVEN MBARONI KWA KUIBIA WAGONJWA SIMU AKIJIFANYA NESI MKUU MUHIMBILI

 By Ngilisho Tv 

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imemkamata , Steven K. Julius kwa tuhuma za wizi wa mali za wa wagonjwa ikiwemo simu za wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kwa kujifanya ni mwajiriwa wa Muhimbili Mloganzila kwa cheo cha Afisa Muuguzi.


Baada ya mahojiano Bw. Julius amekiri kuiba simu tatu ambapo mbili aliziuza kwa mkazi wa Kibamba, na moja ameiuza kwa mtu anyeishi nje ya mkoa wa Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Bw. Julius baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo ya uuguzi (nursing internship) amefanya kazi katika hospitali kadhaa za mkoa wa Dar es Salaam, ambapo alifukuzwa kutokana na vitendo vya kukuika maadili ikiwemo wizi.


Mtuhumiwa amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni kilichopo Kibamba kwa taratibu za kisheria.


Aidha uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unapenda kuihakikishia jamii kuwa inayo mifumo imara ya kiusalama ya kuweza kubaini watu wote, wanaoingia na kutoka hospitalini na ndio maana imeweza kumfuatilia mtuhumiwa huyu na kumkamata.


Post a Comment

0 Comments