Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MKUTANO Mkuu wa Taasisi ya Twariqa Qadiriya Razikia Jailania Taifa, Tanzania ,Umemteua aliyekuwa msemaji wa Taasisi hiyo, Sheikh Haruna Huseni kuwa naibu Katibu Mkuu wa Twarika Taifa,uteuzi ambao umefanyika katika mkutano huo Mkuu ulioketi desemba 24 Mwaka huu.
Sheikh Haruna ambaye anatarajiwa kukabidhiwa ofisi kesho desemba 28,2024 jijini Arusha,alisema amepokea uteuzi huo kwa mikono miwili na kuwashukuru Waislamu kwa ushirikiano wao na kuahidi kutumia uwezo wake wote katika kuwatumikia Waislamu na kuilinda ,amani ya Taifa Letu.
0 Comments