SERIKALI YAREJESHA MNADA WA MADINI YA VITO ,WAZIRI MAVUNDE AZINDUA KWA KISHINDO AAHIDI KUREJESHA MADINI YA WAFANYABIASHARA YALIYOCHUKULIWA NA SERIKALI,TAZAMA PICHA !,

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

SERIKALI imesema itarejesha madini yote kwa wafanyabiashara yaliyokuwa yamehifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT) baada ya kubaki katika mnada wa mwisho uliofanyika Mwaka 2017.

Akiongea katika Hafla ya uzinduzi wa mnada wa Madini ya Vito katika Mji Mdogo wa Mererani , Simanjiro Mkoani Manyara, waziri wa Madini, Antony Mavunde alisema serikali imeamua kurejesha minada ya ndani ya Madini ya Vito ikiwa ni mpango mahususi kurejesha hadhi ya Madini ya Tanzanite na kupandisha thamani kimataifa.


Alisema mnada wa Madini ya vito ilisimama kwa takribani miaka minane iliyopita na kuahidi kutochukua madini ya wafanyabiashara yatakayobaki katika Mnada huo kama ambavyo uvumi umekuwa ukienezwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Madini.

"Uwepo wa minada hii ni chachu ya maendeleo ya sekta ya Madini na kuimarika kwa uchumi wa taifa letu ,minada hii itakuwa  ikiendeshaa kwa njia ya Mfumo wa Kielektroniki kwa lengo la kuweka uwazi na ushindani "



Waziri Mavunde alisema mnada wa Madini ya Vito ulikuwa umesimama kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara ili kuongezeka thamani ya Madini hayo.


Aidha alisema mchango wa madini hapa nchini umeendelea kuimarika katika mwaka wa fedha 2015/16 ambapo sekta ya Madini iliingiza kiasi cha sh, billion 161na baada ya kufanya marekebisho ya sheria na kuanzisha masoko 43 na vituo vya ununuzi 102,sekta hiyo imeanza kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Tanzania.


Alisema fedha iliyoingia katima mfuko mkuu wa serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 ni sh,bilioni 753.Alisema mwaka wa fedha ujao wizara ya madini imejipanga kuingiza kwenye mfuko mkuu wa serikali mapato ya sh,Trilioni 1 katika miezi mitano ya mwaka wa fedha 2025/26.


Hivyo alisema uwepo wa minada ya ndani hapa nchini ina lengo la kuchochea na kuchagiza biashara ya Madini hasa madini ya Vito."Ndio maana serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha inarejeasha hadhi ya Tanzanite ili ikashindane vizuri duniani na moja ya hatua ya kwanza ni urejeshaji wa minada ya ndani nayakimataifa na hatua ya pili ni maonesho ya madini ya vito ili mnufaike na biashara hii"


Mbunge wa jimbo la Simanjiro , Christopher Ole Sendeka pamoja na kuipongeza serikali kwa hatua ya kurejesha minada ya madini ya Vito, alisisitiza kwa kuitaka serikali kutohamisha somo la madini Mererani na kutaka Madini yaendelee  kuuzwa eneo hilo.


Hata hivyo Sendeke alisema bado kuna changamoto ya ukaguzi katika vyumba vya ukaguzi wakati wa kutoka katika ukuta wa Mererani ,akidai watu wanakaguliwa hadi saa nane za usiku akimtaka waziri Mavunde alitolee ufafanuzi jambo hilo.


Waziri Mavunde alimwagiza mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga kushughulikia suala hilo mara moja .


Awali Naibu katibu Mkuu wizara ya Madini Msafiri Mbibo alieleza kuwa madini tofauti yenye uzito wa Gramu 184.06 na Thamani ya sh,bilioni 3.1 yanatarajiwa kuuzwa na kununuliwa kwenye mnada huo.


Alisema mnada huo unafanyika kwa mfumo wa Mtandao ,unahusisha wafanyabiashara wapatao 195 wakiwemo wanunuzi wakubwa 59, wanunuzi wadogo 120,wachimbaji 9 na waongeza thamani 7.


Naye mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Manyara,Peter Toima aliishukuru serikali kwa kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo ilani ya ccm ya mwaka 2020/25 katika sekta ya Madini.


Alisema madini ya Tanzanite yanayopatikana Mkoa wa Manyara lazima yawanufaishe wanamanyara ,hususani katika mjini wa Mererani yanakochimbwa,uwe na maendeleo makubwa kuliko ilivyo sasa .












Ends..
























Post a Comment

0 Comments