Na Joseph Ngilisho ARUSHA
SERIKALI imesema itaendelea kuchukua hatua kuboresha utoaji elimu katika maeneo ya jumla na ya amali ili kuwezesha wadhibiti ubora wa shule na kubuni mbinu mbalimbali zitakazowezesha wanafunzi kuwa na ujuzi ikiwemo fursa za kujiajiri pasipo subiri kuajiriwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Ephraim Simbeye wakati akizungumza kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu kutoka hiyo, Dk Charles Mahera katika mafunzo ya Wadhibiti Ubora wa Shule za Msingi na Sekondari 340 pamoja na waratibu wa mikoa kutoka WyEST kutoka mikoa 26 nchini.
Amesema mafunzo ya amali yanalenga kuboresha elimu nchini ikiwemo mazingira ya kufundishia na kujifunza ili kupata matokeo chanya ya ujifunzaji hususan kwa wanafunzi.
Mikakati mbalimbali imewekwa na serikali katika kuhakikisha wanatumia mbinu za kuhamasisha washiriki kwenye ushiriki wa jamii ikiwemo kuleta maendeleo shuleni , kufanya ufuatiliaji na tathimini ya udhibiti ubora wa shule wa ndani.
Mafunzo ya amali yatasaidia wanafunzi kupata fursa za kujikwamua kiuchumi ikiwemo kufikia Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 pamoja na ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030 ,hivyo maofisa udhibiti ubora shirikianeni na walimu wengine shuleni ili kuleta tija zaidi”
Naye Kamishna wa Elimu, Dk Lyambwene Mtahabwa amesema mafunzo hayo yanalengo la kuweka mpangilio mzuri wa kazi ikiwemo kufundisha na wengine kazini mbinu ufindishaji ili kuleta matokeo chanya katika kusimamia utoaji wa elimu bora.
Mthibiti Ubora kutoka Halmashauri ya Handeni Mkoani Tanga Telesia Kapinga amesema mafunzo hayo yatawapatia elimu ya kujitegemea na kuanzisha viwanda vidogovidogo.
Mafunzo hayo yatafungwa Desemba 02, na yamebeba Kaulimbiu “Utoaji wa Elimu Bora ya Amali hutegemea Tathmini Makini ya Ufundishaji na Ujifunzaji”.
Ends..
0 Comments