RC MWASSA KUWA MGENI RASMI RUZINGA DAY

 RC MWASSA KUWA MGENI RASMI RUZINGA DAY

Mkuu wa mkoa wa Kagera mhe. Fatma Mwassa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la kuchangia maendeleo kata ya Ruzinga Wilayani Misenyi mkoani kagera (Ruzinga day) ambapo atakagua miradi mbali mbali ya maendeleo.


Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo Dkt David Rwechungura wakati akiongea na mtandao huku akiwataka Wananchi wa wa kata hiyo na jirani kujitoza kwa wingi siku hiyo ambapo sherehe hizo itafanyika Desemba 31 Mwaka huu na siku itakayokuwa ni hitimisho la shughuli  za mwaka mzima ambazo zimekuwa zikifanyika tangu mwaka kuanza.


Dkt David amesema kuwa  malengo yao makubwa ni kuendelea kuunga mkono juhudi katika upande wa  sekta ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya ambacho hadi sasa kukamilika kwa ujenzi huo shilingi Milioni 178 zitatumika ambapo  tayari ujenzi huo umeanza na mkandarasi yupo kwenye eneo la mradi.


"Niwaombe wadau wa maendeleo katika kata ya Ruzinga tujikite zaidi katika maendeleo kwani zahanati inayokwenda kuboreshwa  itawahudumia Wananchi na wadau wa maendeleo na wana Ruzinga kwa ujumla kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo"alisema Rwechungura.


Aidha mwekiti huyo aliwaomba wadau hao kutimiza  ahadi zao ili watimize jambo lenye manufaa mbeleni.


Siku ya kuchangia maendeleo kata ya Ruzinga ( Ruzinga day) ufanyika Desemba 31 ya kila mwaka ili kuchagiza maendeleo ya kata hiyo ambapo pia kutakuwepo na michezo mbalimbali ikiwemo  mchezo wa mpira wa miguu, kuvuta kamba, ngoma za asili, kukimbiza kuku pamoja na michezo mbali mbali.

Post a Comment

0 Comments