RC MWASSA AWAKUMBUKA YATIMA KAGERA
Na Lydia Lugakila
Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa ameitumia sikukuu ya Krismas kuwapikia na kushiriki chakula cha pamoja na watoto zaidi ya 200 kutoka vituo vinne Mkoani humo huku akiitaka jamii kujitoa kwa moyo kwa kuendelea kuwasaidia wenye uhitaji.
Mwassa ameshiriki tendo hilo la huruma Desemba 25, 2024 katika ikulu ndogo iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera alipojumuika na watoto hao, wamiliki wa vituo vya kulelea watoto pamoja na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo.
"Mwenyezi Mungu anatuhimiza kwamba kile ambacho ametujalia tukitoe kwa wenye uhitaji na tusifanye kwa kujifaharisha tukifanye kwa nia njema"alisema Mwassa.
Mwassa ameongeza kuwa amebaini wanaowalea watoto hao wana jukumu kubwa na wanabeba dhima kubwa hivyo ni vyema kila mtu kujitoa kwa kitu au vitu walivyobarikiwa badala ya kusubiri umauti kumfika mtu aliyehitaji huduma.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwapongeza wamiliki wa vituo hivyo pamoja na walezi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahudumia watoto huku akiahidi kupanga muda mwingine ambao atakaa na watoto hao na kuwasikiliza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mkoani Kagera Faris Buruhani alimshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa tendo hilo la huruma huku aliwataka wanakagera kuwaombea Viongozi wa namna hiyo.
Mmoja wa watoto walishiriki katika chakula hicho akiwemo Rewina Pius kutoka kituo cha Nusuru Kashai Manispaa ya Bukoba alimshukuru Rais Samia pamoja na Mkuu wa Mkoa huo kwa tendo hilo huku akidai kuwa sio mara ya kwanza kuwaji watoto hao kupitia misaada mbali mbali.
0 Comments