RC MAKONDA APONGEZA WANANCHI WALIOMBURUZA KWENYE MATOPE DIWANI MBISE NA MWENYEKITI WAKE WA MTAA,AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUWASHUGHULIKIA VIONGOZI WENGINE WAZEMBE,AKERWA BILIONI 20 ZA JIJI LA ARUSHA KUREJESHWA SERIKALI KUU VIONGOZI KUKALIA MAJUNGU ,TAZAMA PICHA!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewapongeza wananchi wa kata ya Muriet,mtaa wa Kimara jijini Arusha kwa ujasiri wa kujichukulia sheria mkononi nabjuamua kuwaburuza kwenye Matope Diwani wa kata hiyo Francis Mbise na viongozi wengine wa mtaa kwa kushindwa kusimamia changamoto ya ubovu wa miundo mbinu ya barabara inayosababisha adha kwa wananchi hao.
 






"Jana niliona Crip moja ikisambaa kuna wananchi wamewaburuza kwenye matope viongozi wao ,hongereni mno,wamemburuza diwani wao,wakamburuza na mwenyekiti wa mtaa nawapongeza sana kwa sababu hawa viongozi lazima kila mmoja awajibike hatuwezi kuwa na viongozi halafu wananchi wanashida wao hawawajibiki"

Aidha Makonda amewataka wananchi ambao maeneo yao ni machafu, kukusanya uchafu na kwenda kumwaga kwa viongozi wao ambao wameshindwa kusimamia suala la safi katika jiji la Arusha .

Makonda ametoa pongezi hizo mbele ya naibu waziri mkuu Dotto Biteko,wakati wa ufunguzi wa  kongamano la 15 la wataalamu wa ununuzi na ugavi linaloendelea jijini Arusha na kusisitiza kuwa ataendelea kuwahamasisha wananchi wawashikishe adabu viongozi wazembe.

Alisema mwaka wa fedha 2022/24 halmashauri ya jiji la Arusha imerudisha fedha serikali kuu takribani bilioni 20 kwa sababu viongozi wavutana,majungu ,fitna na ushirikina halafu wananchi wanakosa maendeleo ,wanafunzi wanakosa madarasa ,matundu ya vyoo halafu fedha zinarudishwa.

"Nawaagiza wananchi katika jiji la Arusha  wakiona Mbunge,Diwani na viongozi wa mtaa wasiofanyakazi yao wawazomee na kuwaburuza kwenye matope ili wapate nidhamu ya kuwatumikia wananchi.

"Na wasiishie tu kuwazomea hata wakikuta kwenye mtaa mchafu, wananchi wa Arusha nawahamasisha wachukue huo  uchafu na kwenda kumwaga kwa viongozi hao "

Jana majira ya asubuhi katika Mtaa wa Kimara ,kata ya Muriet jijini hapa,makuminya wananchi walijikusanya na kufunga barabara kwa mawe na baadaye waliamua kuwaburuza viongozi wao kwenye matope wakiwalazimisha kupita kutokana na kero ya muda mrefu ya ubovu wa barabara kujaa maji na kutopitika kirahisi.

Jambo hilo lilimlazimu mkuu wa wilaya ya Arusha, Feliciani Mtahengerwa na meneja wa Tarura Mkoa pamoja na polisi kufika eneo la tukio kwa lengo la kutuliza ghasia za wananchi hao .




Ends









Post a Comment

0 Comments