RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Aidha aliyekuwa Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba ameteuliwa kuwa Balozi, na atapangiwa kituo cha kazi, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Mosses Kusiluka imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dk James Kilabuko kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu).
Advertisement
Dk Stephen Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji.
Dk Suleiman Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, aidha, Balozi Dk John Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi.
0 Comments