PENDEKEZO LA KUFUTWA KWA MAMLAKA YA MJI MDOGO NGARAMTONI LATUA KAMATI YA USHAURI YA MKOA (RCC)

By Ngilisho TV


Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kimepokea mapendekezo kutoka Halmashauri ya Arusha yaliyojielekeza kufutwa kwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa  Ngaramtoni, kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa Mamlaka hiyo, kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Desemba 18, 2024.



Akiwasilisha mapendekezo hayo kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Suleiman Msumi, amesema uamuzi huo unatokana na malalamiko ya wananchi ambao wamedai  gharama ya huduma za uendeshaji wa Mamlaka ya mji huo mdogo kuwa kubwa


Amesema malalamiko hayo yalitolewa kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara ikiwemo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Chtistian Makonda aliyembatana na Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi Mkoa wa (CCM) kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi,ambapo mionhoni mwa kero, wananchi walilalamikia gharama kubwa  uendeshaji wa Mamlaka ya mji mdogo na kuomba ifutwe.


Aidha, amebainisha kuwa, Halmashauri ilipokea malalamiko ya wananchi ambao walionyesha kuwa hawakotayari kuwepo kwa Mamlaka hiyo na kulazimu halmashauri kuanza mchakato wa vikao vya maoni kuanzia ngazi za vijiji na hatimaye kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya fedha na Baraza la Madiwani na hatimaye kufikishaa kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya (DCC)


Msumi ameendelea kueleza kuwa, baada ya vikao hivyo kutoa pendekezo hilo,  halmashauri imewasilisha kwenye kikao Kamati ya Ushauri Mkoa ili kuwasilisha ombi hilo Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI )kwa hatua zaidi.


Akichangia hoja hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mhe. John Maha, ameomba halmashauri zao zipandishwe hadhi na kuwa manispaa  kwa kuwa kuna faida zikipandishwa hadhi na kuwa manispaa.


Ameshauri iundwe Kamati ya Mkoa itakayokuwa ikipendekeza halmashauri kupandishwa hadhi na kuongeza kuwa hata Karatu nao wana Mamlaka ya mji mdogo.


Ends..

Post a Comment

0 Comments