NSSF YATOA MSAADA WA PIKIPIKI 20 KWA MKOA WA ARUSHA,RC MAKONDA AAHIDI WANACHAMA KIBAO KUJIUNGA NSSF AKABIDHIWA PIKIPIKI NI VITENDEA KAZI VYA JESHI LA POLISI KATIKA KUBORESHA ULINZI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF,umekabidhi pikipiki 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Paulo Makonda ikiwa ni hatua ya kuunga mkono mpango wa mkuu huyo kuboresha utendaji kazi wa jeshi la Polisi Mkoani humo ili kuimarisha ulinzi sekta ya utalii.

Pikipiki hizo ni Miongoni mwa Pikipiki 60 zilizokabidhiwa na wadau mbalimbali akiwemo Mch.Boniphace Mwamposa wa kanisa la Arise and Shine, aliyetoa msaada kama huo, mfanyabiashara Fazal ambaye pia alitoa pikipiki 20 kwa mkuu huyo wa Mkoa katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu huyo na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa NSSF ,meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma NSSF,Lulu Mengele alisema msaada huo umekuja baada ya kupokea  ombi kutoka ofisi ya Mkuu wa  mkoa Arusha kwa ajili ya kulisaidia jeshi la polisi kufanyakazi zake  kwa ufanisi  zaidi katika kulinda wananchi na rasilimali zao .

"Tulipata Ombi kutoka ofisi yako tuliona ni muhimu sana na sisi NSSF kuweza kushiriki knowkatika kuchangia pikipiki kwa jeshi la Polisi ambalo linafanyakazi kubwa ya kulinda usalama wa raia na mali zake.

Alisema NSSF imetoa msaada wa pikipiki 20 kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa jeshi la Polisi ikiwa ni hatua ya kuimarisha ulinzi katika sekta ya utalii mkoani hapa hatua ambayo itasaidia pia kupata wanachama wapya wa mfuko huo.

Aidha Mengele alimshukuru RC Makonda na viongozi wengine waliochangia mfuko huo kuweza kuandikisha  wanachama wengi kutoka kampuni mbalimbali binafsi,pia aliahukuru mpango wa mkuu huyo wa mkoa utakaofanikisha kuwafikia wananchi wengi na kuweza kujiandikisha katika mfuko huo wa Nssf.

"Tutahakikisha kila mwananchi mwenye kipato  anaweza kutibiwa katika hospitali yoyote anayotaka  kwa mchango wa kuanzia sh,30,000 na sh,52,000 kwa familia "Alisema 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda,aliwashukuru wadau wa maendeleo kwa kuchangia vitendea kazi kwa jeshi la polisi ambapo hadi sasa polisi wamepata pikipiki 120 ,wakitanguliwa na pikipiki 60 walizokwisha patiwa.

"Leo tumepokea msaada wa pikipiki 60 zikiwemo 20 zilizotolewa na Mfuko wa NSSF,20 zilizotolewa na Mchungaji Mwamposa na 20 Zilizotolewa na mfanyabiashara Fazal wa kampuni ya Utalii ya Leopard na hawa wadau hatuwaombi ila wanaguswa na kuomba kuchangia ".

Makonda aliahidi kwa Nssf kuwa Mkoa wa Arusha utaendelea kuvunja rekodi kwa kuongiza wanachama kutokantaaisis rasimi na zaizokuwa rasimi.

Aliwataka wakuu wa wilaya kupitia program ya miezi mitatu waliojiwekea kuhakikisha wanasajili wanachama wapya wapatao elfu 10 kila wilaya ikiwemo kuwapatia elimu ya kujiunga na mfuko huo.

Aidha alisema Polisi wanafanyakazi  kubwa katika mazingira mgumu hadi usiku kuhakikisha wananchi na mali zao wanabaki salama,aliwataka wananchi waendelee kushirikiana na polisi ili kutokomeza ujambazi na
 uhalifu.







Ends..














 

Post a Comment

0 Comments