MEYA ARUSHA AFAFANUA HOJA YA UBOVU WA BARABARA PAMOJA NA UJENZI HOLELA KATIKA JIJI LA ARUSHA,AZUNGUMZIA ONGEZEKO LA MAPATO

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

SIKU moja mara baada ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Feliciani Mtahengerwa kutoa karipio kali kwa watendaji wa halmashauri hiyo kuhusu kukwamisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na ujenzi holela,meya wa jiji hilo, Maximum Iranghe ameibuka na kuwataka wananchi kuwa na imani na serikali yao.


Iranghe akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu hoja zilizoibuliwa katika baraza la Madiwani hapo jana kuhusu hoja ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa vyumba vya madarasa, kujenga na kuboresha vituo vya afya na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo.

Alisema baraza la madiwani lililofanyika Nov 6 jijini arusha, limeazimia manunuzi ya greda na mitambo kwa ajili ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara na mitalo inayoendelea, ambapo imetengwa kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya manunuzi ya mitambo tajwa.


Aidha ameongeza kuwa, baraza limeelekeza utoaji wa vibali vya ujenzi unaozingatia sheria pamoja na maendeleo ya mji, sehemu ya jiji ambayo ina mitaa kuu ya biashara na majengo makuu ya umma ikijumuishwa na viwanda, makazi, biashara, utawala na matumizi (CBD).


“Baraza la madiwani limeazimia upangaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza, uzingatie umbali na urahisi wa usafiri ili kupunguza adha kwa wanafunzi na kuboresha kiwango cha elimu na ufaulu, miradi ya ujenzi wa madarasa kukamilika kwa wakati, sambamba na ujenzi wa vivuko ili kuunganisha mitaa ya jiji na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla” amesema Iranqhe.


Hata hivyo amesema baraza limeelekeza uitishwe mkutano wa dharura wa baraza la madiwani kwa kuwashirikisha TARURA TANROADs na AUWSA ili kujadili kwa kina changamoto ya barabara kwenye mitaa ya jiji la arusha.

Vile vile amewakumbusha wananchi kuendelea kupanda miti, kufanya usafi katika maeneo yao, wadau wa maendeleo kuendelea kufunga taa walau mbili mbele ya ofisi au makazi yao na kupamba mji kwa miti ya krismas msimu huu wa sikukuu.


Kadhalika Meya alisema suala la ujenzi holela,vibali  havitolewi na madiwani, vinatolewa na watendaji wa halmashauri hivyo na sio sawa kuwalaumu madiwani kuhusiana na suala hilo na kusisitiza kuwa vinali vya ujenzi vitolewe kwa kufuata sheria na kanuni za ujenzi.

Ends..

Post a Comment

0 Comments