Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WANACHAMA wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,zaidi ya 50 katika kata ya Kaloleni jijini Arusha wamekihama Chama hicho na kutimkia chama cha Mapinduzi CCM wakidai kuvutiwa na kasi ya Maendeleo inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hasani .
Wafuasi hao wa Chadema akiwemo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa mtaa wa mita miambili,Chacha Motabo,walirejesha kadi zao na kupokewa na diwani wa kata hiyo, Maximum Iranghe ambaye pia ni meya wa jiji la Arusha.
Akiongea kwa niaba ya wenzake ,Chacha Motabo alisema haoni haja ya kuendelea kubaki chadema kutokana na migogoro inayoendelea na kwamba chama hicho kinapoteza mvuto kwa wananchi na wamachama wake.
"Mimi na wenzangu kama mnavyowaona tumeamua kurudi nyumbani na leo tumejiunga na CCM ,tumevutiwa na maendeleo yanayofanywa na rais Samia Suluhu,pia migogoro inayoendelea ndani ya chadema kuna dariri ya kugawanyika ndio maana imetulazimu kuondoka na kujiunga na ccm"Alisema Chacha.
Akiwapokea wanachama hao wapya meya wa jiji la Arusha, Maximilian Iranghe aliwashukuru kwa uamuzi wao akisema hawatajutia na kuongeza kuwa heshima imrudie Rais Samia yeye ndo ameleta maendeleo yaliyowashawishi kujiunga na ccm.
Meya alisema kabla ya wanachama hao kujiunga na ccm, kata hiyo ilikuwa haina utulivu kutokana na wanachama hao wa chadema kuendesha siasa za mara kwa mara na kufanya wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo na kukalia siasa.
Ends..
0 Comments