NGORONGORO YAITA WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZAKE , YAZINDUA KAMPENI KABAMBE MSIMU WA SIKUKUU KUJIONEA VIVUTIO NDANI YA HIFADHI ZAKE

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MAMLAKA ya Hifadhi ya  Ngorongoro (NCAA)imezindua Kampeni ya kuhamasisha utalii wa Ndani msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka (Merry $ Wild Ngongoro A waits), kwa ajili ya kuwezesha watanzania kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kujionea vivutio mbalimbali .

Akiongea na vyombo vya habari, jijini Arusha,kamishna msaidizi Mwandamizi idara ya utalii na masoko (NCAA),Mariam Kobelo,alisema kuwa  kampeni hiyo inaanza leo Desemba 4 hadi January 4 ,2025.


Alisema kampeni hiyo imelenga kuhamasisha watalii wa ndani  kuvijua vivutio katika maeneo ya hifadhi na kujenga tabia ya kutembelea hifadhi zinazosimamiwa na mamlaka  hiyo.

"Mamlaka ya Ngorongoro tumeamua kuanzisha Kampeni hii kwa mwaka huu ili kuwezesha watanzania wengi kuweza kutembelea katika maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro ili kujionea na kushuhudia vivutio vizuri vinavyopatikana ndani ya maeneo ya uhifadhi "

Alisema idadi ya wataliinwa ndani wanaotembelea vivutio vya imezidi kuongezeka na takwimu zinaonesha kwamba kuanzia julai hadi hadi Novemba mwaka huu 2024 watalii wa ndani wamefikia zaidi ya 200,000.

Alisema idadi hiyo bado haitoshi ndio maana mamlaka hiyo imebuni kampeni ya kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio katika hifadhi ya Ngorongoro yenye vivutio vingi ambavyo watanzania wengi bado hawajavifahamu

Aliyataja baadhi ya maeneo yenye vivutio kama urithi wa utamaduni Olduvai,Kreta ya Empakai na Olmoti na mlima wa tatu kwa  urefu Tanzania ulitwao Loromalasi.

Pia alisema watanzania watakaotembelea hifadhi watanufaika na vivutio vya msimu wa Ndutu kujionea idadi kubwa ya Nyumbu waliojerea nchini kujifungua kabla ya hawajahama tena kwenda hifadhi ya Masai  Mara nchini Kenya.

Alisema Mamlaka ya hifadhi ya  Ngorongoro kwa kushirikiana na wadau wa utalii,kampuni ya Smile Safari wameandaa vifurushi vitakavyowawezesha watanzania kuchagua ili kuwawezesha kutembelea vivutio hivyo.


Alisema watalii wa ndani watapaswa kuchagua vifurushi maalumu vya aina tatu ambavyo ni  Kifurushi cha Faru  
 Gharama: Shilingi 450,000 kwa kila mtu  
   - Utalii wa siku mbili (24-25 Desemba 2024)  
   - Huduma: Kiingilio, malazi, chakula, muongoza watalii, usafiri na huduma ya picha.  

2. Kifurushi cha Tembo 
   - Gharama: Shilingi 130,000 kwa kila mtu  
   - Utalii wa siku moja (Day Trip)  
   - Huduma: Kiingilio, chakula, muongoza watalii, usafiri na huduma ya picha.  

3. Kifurushi cha Chui
   - Gharama: Shilingi 85,000 kwa kila mtu  
   - Utalii wa siku moja (Day Trip)  
   - Huduma: Usafiri wa basi, kiingilio, chakula, muongoza watalii na huduma ya picha.

Katika utekelezaji wa Kampeni hiyo NCAA inatumia vikundi mbalimbali vya Sanaa vikiongozwa na vijana wa _Action Rollers Skates_ na Makachu Jumpers ambao  watakuwa  katika mitaa mbalimbali kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia tarehe 4 hadi 16 Desemba, 2024.


Katika utekelezaji wa kampeni ya kuhamasisha utalii, wananchi wote wanakaribishwa kutembelea vivutio vilivyoko katika eneo laa hifadhi ya Ngorongoro na wanaweza kuchagua kifurushi chochote kati ya vitatu vilivyotangazwa kwa kupiga namba za simu 0755 559013 ili kuweka  nafasi (booking).


Akizindua kampeni hiyo katibu Tawala msaidizi idara ya Uchumi  na uzalishaji Mali,Daniel Loiruck akimwakilisha katibu Tawala Mkoa wa Arusha,alisema mpango wa kuboresha sekta ya utalii Mkoa wa Arusha upo mbioni.

Alisema Mkoa unaunga mkono kampeni hiyo ya kuhamasisha watanzania kupenda kutembelea vivutio vya utalii katika hifadhi mbalimbali chini.






Ends .


Post a Comment

0 Comments