MAJAJI NA MAHAKIMU ZAIDI YA 300 KUJENGEWA UWEZO ARUSHA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MAJAJI na Mahakimu zaidi ya mia tatu wanaotarajiwa kukutana mkoani Arusha kuanzia kesho na watapata fursa ya kujengewa uwezo katika maswala ya kuendesha Kesi za jinai,madai na migogoro ambapo lengo kuu ni kuhakikisha wanamaliza na kutatua migogoro kwa haraka .


Aidha migogoro inapotatuliwa kwa haraka sana watu wanatoka kwenye migogoro mahakamani na kwenda kwenye shughuli zao za uzalishaji na hiyo ni faida kwa wananchi na ndilo lengo kubwa .


Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Manyara na Rais wa Chama cha majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) John Kahyoza ,wakati.akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo.


Jaji Kahyoza amesema kuwa, wataweza kuangalia swala zima la migogoro ya kazi katika kuangalia migogoro ya kazi inatatuliwa vipi kwani kanuni mojawapo ya mwajiri ni kuajiri na kuondoa watu kazini na kama mwajiri hawezi kuwa na haki ya kufukuza watu watakuwa wazembe kazini .


“Kwa hiyo eneo hilo tumeona na lenyewe tuliangalie namna wenzetu wamefanya vizuri na wamefikia wapi kwani nchi kama nchi itakuja kunufaika pale ambapo migogoro itatatuliwa kwa haraka na wananchi kwenda kufanya shughuli za uzalishaji Mali.”amesema .


Amesema kuwa ,lengo kubwa la maboresho wanayofanya mahakamani na hasa kwa Tanzania ni kuongeza imani ya wananchi kwa mahakama ndio lengo kubwa la kwanza na hata hii elimu tutakayopata wiki nzima tunataka kuona tukitoka hapa wananchi wawe na imani zaidi kwa mahakama ndio maana wanaungana na wenzetu na kupata ujuzi zaidi.


Aidha ameongeza kuwa, wanataka kuona wamepunguza muda wa mashauri kubaki mahakamani ndio lengo la mambo yote hayo ndio maana wanaangalia taratibu za kuendesha mashauri yao ya migogoro ya kazi ,jinai, madai unakuta mtu anawekwa ndani miaka miwili hadi saba anakuja kutoka ndani na anakuwa hawezi tena kuzalisha na nguvu ile ile .


“Zamani ulikuwa ukikutwa na kesi ya mauaji zamani waliita kama kombe la dunia kwani unakaa muda mrefu ila siku hizi mambo yamebadilika mtu anatenda kosa la mauaji na mwaka huu huu anahukumiwa huko ndo tulipofikia sasa kama una hatia una hukumiwa kunyongwa kama huna hatia unarudi uraiani ukafanye kazi zako nyingine hayo ndio malengo makubwa kwani hatuwezi kuzuia migogoro ila ikitokea inapaswa itatuliwe haraka sana “amesema Jaji Kahyonza. 


Aidha ameongeza kuwa ,kuwepo kwa matumizi ya Tehama mahakamani umesaidia sana kuboresha huduma kwa wananchi ambapo yamepunguza viashiria vya rushwa na hisia za mtu kusema kuwa anazungushwa ili atoe rushwa.


Jaji Kahyonza amefafanua kuwa matumizi ya Tehama yamesaidia sana kupunguza malalamiko ya nakala za hukumu ila kwa sasa hivi nakala hizo zinakufuata moja kwa moja ulipo kupitia barua pepe na imesaidia sana kupunguza upotevu wa mafaili ambao ulikuwa ukilalamikiwa kwa kiwango kikubwa sana.


Amesema kuwa, kupitia matumizi hayo ya Tehama imesaidia sana uharakishaji wa usikilizaji wa Kesi hivyo wameweza kuboresha huduma kwa kutumia Tehama na wananchi wanafaidi. 


Ends..

Post a Comment

0 Comments