KISHINDO CHA UMK 2025 KUISHANGAZA JAMII

 Kishindo cha UMK 2025 kuishangaza jamii

Na Lydia Ezra Lugakila

Misenyi

Umoja wa Maendeleo Kikukwe(UMK) umejipanga kuhakikisha mwaka 2025 wanakuja ki vingine katika kuleta maendeleo  Kijijini kikukwe Wilayani Misenyi mkoani kagera.


Akizungumza Desemba 27, 2024 katika sherehe za umoja wa maendeleo kikukwe (UMK) zilizofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Kanyigo Bi Magreth Kyai ambaye ni katibu mkuu wa umoja huo amesema kuwa  katika mkutano Mkuu walioanza nao kabla ya sherehe hizo wamejadili mambo mazito kwa ajili ya Kijiji hicho huku Mwaka ujao 2025 wameweka mikakati  mbali mbali ambayo itaishangaza jamii.


Bi Kyai amesema kuwa watatakiwa kwenda katika jamii kuwaelimisha wana jamii katika Kijiji Cha kikukwe ili waelewe vizuri nini maana ya Kijiji kikukwe hii ni kutokana na baadhi ya watu wengi kutokuwa na uelewa na mambo ya maendeleo badala yake wanaelewa masuala ya sherehe na misiba tu.


"Unakuta watu hawagusi mambo ya maendeleo hii ni changamoto najua huu ni Mwaka wa nne tangu tumeanza hivyo kikukwe day lengo letu 2025 tunakuja kivingine katika kuchagiza maendeleo" alisema katibu mkuu huyo.


Aliongeza kuwa walishajenga bweni la wasichana shule ya Sekondari Kanyigo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ambali na Serikali ambapo ujenzi huo umefikia hatua ya linta na wamejipanga kuingia kwa nguvu kubwa kwa Mwaka 2025 ili kupaua jengo hilo.


Alisema kuwa umoja huo wa maendeleo katika miundo mbinu wameandaa kwa Mwaka 2025 wanaweka juhudi katika ujenzi wa bweni ambapo kamati ya uchumi wamejipanga kuendelea kuhamsisha watu wengi kuchukua miche ya parachichi na tayari wamepanda majumbani mwao kwa ajili ya kuhamasisha kilimo.


Aidha ameongeza kuwa wamejadili na kupanga katika kikao hicho kipaumbele chao kikubwa 2025 ni kwa ajili ya kumalizia  kupaua paa huku akitumia fursa hiyo kuwaomba Wananchi kuguswa ili kuweka nguvu kumalizia bweni hilo.


"Tumewaomba Serikali ya Kijiji kushirikiana na sisi ambao tunaishi nje ya Mkoa na kijiji cha kikukwe ili waishio nje ya Nchi na wao waweka nguvu sana Mwaka 2025 tuwe bora zaidi"alisema Bi Magreth.


Aidha alisema kuwa Shilingi Milioni 25 zinahitajika ili kukamilisha kazi hiyo hivyo kupitia mkutano Mkuu wamechaguliwa wajumbe wa Umoja huo kwenda katika vitongoji kusaidiana na Viongozi kuhamasisha watu kuongeza nguvu kuchangia kiasi cha Shilingi 10,000 kwa ajili ya watoto wao wanaoisaka elimu.


Alisema kuwa  kumalizika kwa jengo hilo kutagharimu  shilingi milioni 50 na kufikia linta kumegharimu Shilingi Milioni 38 na bweni hilo litabeba wanafunzi wa kike wapatao 150.


Aliwapongeza wana kikukwe kwa mwitikio wao mzuri tangu wameanza huku akisisitiza kuwa suala la siasa ni mwiko kuingizwa katika kazi hiyo hivyo wamejipanga vizuri katika kuweka misingi bora.

Hata hivyo kwa upande wake mwakilishi wa Mwenyekiti wa Umoja wa maendeleo kikukwe Jonas Majula amewashukuru wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na Wananchi waliojitokeza katika sherehe hizo huku akiahidi kuwa Mwaka 2025 sherehe hizo zitaanza wiki moja kabla ambapo wataanza na michezo mbali mbali ikiwemo mbio za baiskeli wanaume kwa Wanawake na kwa mahindi wa kwanza wapili na watatu watapata zawadi.


Hata hivyo Majula aliongeza kuwa kutakuwa pia na mpira wa miguu  hivyo watu waanze kujiandaa huku akiwahimiza wananchi kuchangia maendeleo ya shule ya Sekondari Kanyigo ili kuwapa nguvu watoto wao na kuongeza ufaulu.


Kikukwe Day huadhimishwa kila ifikapo Desemba 27 ya kila mwaka.

Post a Comment

0 Comments