JUMUIYA YA WAISLAMU ARUSHA (AMU), YAMBURUZA MAHAKAMANI KABIDHI WASII MKUU RITA,ASHINDWA KUTOKEA MAHAKAMANI JAJI ATOA AGIZO

Na Joseph Ngilisho ARUSHA

JUMUIYA ya Waislamu Arusha (Arusha Muslim Union)(AMU),imemfikisha Mahakamani Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa RITA,Frank Kanyusi,wakiitaka Mahakama kumzuia kuingilia migogoro ya ndani ya Waislamu.


Kesi hiyo ambayo ipo mbele ya jaji  Sylvester Kainda wa Mahakama Kuu Arusha, wakili anayewakilisha jumuiya hiyo, Mustapha Akunaay alisema wateja wake wamefungua shauri hilo kuitaka mahakama kumwamuru Kabidhi Wasii Mkuu kutoingilia masuala ya ndani ya dini hiyo na kutoa amri zinakinzana na masuala ya dini hiyo.




Pia ameiomba Mahakama imlazimishe Kabidhi Wasii Mkuu kufuta uamuzi wake wa kuunda kamati ya kushughulikia mgogoro wa jumuiya hiyo.


Hata hivyo katika shauri hilo lililokuja kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, mshtakiwa  hakuwepo mahakamani licha ya Kupelekewa wito wa Mahakama (summonse) .


"Mh Jaji tulipeleka Summonse kwa mshtakiwa na ikapokelewa na kugongwa mhuri lakini tunashangaa hayupo katika mahakama yako leo"



Jaji Kainda baada ya kusikiliza maelezo ya upande mmoja aliahirisha shauri hilo hadi February 21,2025 kwa maelekezo kwamba mshtakiwa apelekewe wito nyingine wa kumtaka afike mahakamani hapo bila kukosa.


Jumuiya hiyo ya Waislamu haikubaliani na kamati iliyoundwa na Mkurugenzi huyo wa RITA ambayo imewajumuisha waumini kutoka baraza la waislamu Tanzania Bakwata ambao wanamgogoro wa kugombea mali na AMU.


"Sisi hatutaki Bakwata wajumuishwe kwenye kamati ya kushughulikia mgogoro wetu wa ndani ,Bodi ya wadhamini ya AMU ina Utata wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuhusiana na umiliki wa nyumba ya biashara iliyopo kwenye eneo la kiwanja namba 34 kitalu G eneo F katika jiji la Arusha "

Mmoja ya viongozi wa AMU , Mustapha Kihago alisema kuwa katika kikao kilichoketi katika ukumbi wa halmashauri ya jijini la Arusha, kati ya Kabidhi Wasii Mkuu Frank Kanyusi viongozi wa AMU ,Bakwata na watendaji wa serikali, Kanyusi aliwatangazia juu ya uwepo wa kamati aliyoiunda ya kushughulikia mgogoro wa kugombea mali, kamati ambayo iliwajumuisha Bakwata ,jambo ambalo alisema hawakuwa wamekubaliana bali aliwalazimisha akitumia nafasi yake.


"Tumeamua kwenda mahakamani kupinga mamlaka ya Kabidhi Wasii Mkuu kuingilia mambo ya ndani ya mgogoro wa jumuiya ya Waislamu Arusha kwa sababu tumebaini anatumika na Bakwata ambao tunamgogoro nao wa muda mrefu ambao poa ameshindwa kuutatua"


Ends..
















Post a Comment

0 Comments