IAA YAJITANUA KIMATAIFA YAWEKEZA BILIONI 10 KAMPASI YA BABATI,YAJIPANGA KUPOKEA WANAFUNZI ZAIDI YA ELFU 40,MKAKATI WA KUBADILISHANA WALIMU NA WANAFUNZI KATIKA NCHI ZA CHINA NA UINGEREZA UPO JIKONI!

 Na Joseph Ngilisho BABATI.


CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA)kimeweka bayana mpango wake wa kujitanua kimataifa kwa kuanza kubadilishana ujuzi na walimu na wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya kimataifa duniani.

Aidha chuo hicho katika kampasi ya Babati Mkoani Manyara, kimewekeza kiasi cha sh, bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa miradi muhimu ya Majengo makubwa  ili kupokea wanafunzi takribani elfu 10 hadi elfu 15 katika kipindi cha  miaka mitano ijayo.

Akiongea na waandishi wa habari pamoja na wahariri waliotembelea miradi hiyo,mkuu wa chuo  hicho,Prof Eliamani Sedoyeka alisema kwa chuo , kina jumla ya Kampasi Tano  , Arusha ,Babati, Dar es salaam,Songea na Dodoma na wapo katika maboresho makubwa ya kufikisha takribani wanafunzi elfu 40 hadi elfu 50 katika miaka mitano ijayo.

Alisema mradi wa Kampasi ya Babati wenye eneo lenye ukubwa wa hekari 65 awamu ya kwanza ,unahusisha ujenzi wa majengo ya  Madarasa ,  Mabweni(Hostel) na Cafeteria ikiwa ni pamoja na ujenzi viwanja nane vya michezo  vitakavyotumika kama kituo cha kufundisha elimu ya michezo ya kimataifa kitakachogharibu takribani milioni 500 ili kwendana na kasi ya maendeleo ya michezo nchini.
,

"Awamu ya kwanza ya mradi katika Kampasi yetu ya Babati  inahusisha ujenzi wa Madarasa , Hostel, Cafeteria na ujenzi wa Viwanja vinane vya michezo na mpaka sasa  ujenzi wa  Mabweni upo asilimia 75 na nusu ya Mabweni yamekamilika kwa  asilimia 95 na Jengo la Cafeteria lipo asilimia 50 na tunatarajia kukamilisha katika kipindi cha mwaka huu wa fedha 2024/25 na tayari wanafunzi zaidi ya 300 wanaosoma"

"Awamu ya pili kupiti fedha za mradi wa kitaifa wa Elimu ya juu (HEET) tunatarajia kuanza ujenzi eneo la mbele la chuo ,jengo la Utawala na jengo la Library na Kompyuta"Alisema 

Alifafanua kwamba Kampasi ya Babati na Songea malengo yake ni kutengeneza Kozi kwa vijana wa kitanzania kupata ujuzi unaoendana na Uhalisia wa mazingira ya wakazi wa eneo husika ikiwemo Ufundi wa Seremala na Vyuma.

Prof, Sedoyeka aliwataka wakazi qa mji wa Babati kichangamikia kuwekeza katika ujenzi Hostel ili kunufaika na uwepo wa chuo hicho kwa kuuza vyumb vya kulala.

Alisema mpango ukakati wa chuo cha Uhasibu Arusha ni kujitanua kimataifa ,kuanzisha mashirikiano  na vyuo mbalimbali vya kikataifa duniani na tayari tumeshafanya safari ya kimkakati katika nchi za Sudani kusini, Comoro China na Uingereza kuona namna ya kutengeneza mahusiano ili kubadilishana uzoefu katika kozi mbalimbali kwa kubadilishana walimu na wanafunzi.

"Kwa sasa tunaendelea kuboresha miundombinu yetu ya  madarasa ili kuendena na mandari ya kimataifa katika maeneo ya kulala ,kula na kusomea  na tayari tumeanza kujipanga kwa madarasa yetu kuwa Smarti na mipango ya kuunganisha Kampasi zote  na vyuo vingine nje ya nchi ili tutakapoanza mashirikiano, walimu wataweza kufundisha huko waliko sio lazima wasafiri"

Naye meneja wa Kampasi ya Babati dkt, Eliakira Nnko alisema kuwa kampasi hiyo kwa sasa inachukua wanafunzi wa elimu ya ngazi ya cheti na diploma na wanajumla ya wanafunzi zaidi ya 300 wanaolala katika hosteli ambazo zimekamilika zikiwa na ubora wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Bodi wa chuo cha (IAA)Mwamini Tuli,alisema jukumu la bodi ni kuhakikisha wanatembelea miradi ya chuo ili kujiridhisha na kile wanachokubaliana kuhakikisha kinatumika kama ipasavyo kwa manufaa ya umma.

"Baada ya kutembelea tumeridhika na maendeleo ya miradi ya ujenzi ila kama tutabaini kunachangamoto za matumizi ya fedha huwa tunaomba vyombo mbalimbali kuchunguza iwapo kama kuna ubadhilifu wa fedha.








Ends...













Post a Comment

0 Comments