Na Joseph Ngilisho ARUSHA
HOSPITALI ya rufaa ya ALMC ya jijini Arusha, chini ya Program yake ya Tiba Shufaa na Huduma ya Faraja imeendelea kutoa hudumia kwa watoto waliofiwa na wazazi wao kutokana na magonjwa yasiyotibika(Kusendeka) yakiwemo Saratani na Ukimwi.
Tangu kuanzishwa kwa kitengo hicho watoto na watu wazima wenye magonjwa yasiyotibika zaidi ya 6000 wamehudumiwa kupitia program ya Tiba shufaa.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa utoaji elimu ya Saikolojia na ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto hao,mratibu wa program hiyo,Tumaini Kweka alisema huduma ya Tiba shufaa hutolewa nyumbani kwa mhusika ama hospitalini na katika kitengo hicho.
Alisema kuwa huduma hiyo ilianza mwaka 1999 kwa kutoa huduma ya kimwili,kiroho ,kiakili na kijamii . Ambapo wagonjwa wanaowapatia hudumia hii ni wale wenye magonjwa ya kusendeka(Yasiyotibika)kama Ukimwi,Saratani,Moyo,Kisukari ,Kupararaizi,Kifafa na kwamba wanaopatiwa huduma hii ni pamoja na wale waliozidiwa kwa kupewa dawa.
Alisema hadi sasa tangu kuanza kwa huduma hiyo wagonjwa wapatao 6000 wameshawapatia huduma hiyo kwa kuwatembelea majumbani ,kuwapa faraja ,tiba na huduma za kiroho.
"Siku ya leo tumekusanya watoto waliofiwa na wazazi wao kwa magonjwa hayo ,ambao wanaishi katika mazingira magumu ili tuwapatie faraja ,elimu ya namna ya kuishi ili wasikate tamaa katika maisha yao"Alisema.
Naye muuguzi wa afya ya jamii Paulina Natema,alisema kitengo hicho kinapokea watoto wenye mahitaji maalumu katika jamii, alisema huduma wanazotoa katika kitengo hicho ni pamoja na kutoa tiba kupitia msaada wa wafadhili .
Alisema mmoja ya watoto wanaopatiwa huduma,baraka...kutoka Odonyo Sambu alikuwa akisumbuliwa na kidonda kwenye mguu na baadaye kugundulika kuwa kidonda hicho kinaweza kusababisha kansa ndipo kitendo hicho kilipogharamia matibabu ya kukatwa mguu kwa gharama ya sh,milioni 3 zilizogharamiwa na program ya kitengo hicho.
Baadhi ya watoto wanufaika wa program ya Tiba shufaa,Juliana Titus ,anbaye amepoteza mzazi wake kwa ugonjwa wa saratani alisema anamshukuru mungu kwa huduma wanayopatiwa inawafanya wajisikie bado wanawazazi wao.
Ends..
0 Comments