Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Balozi dkt Pindi Chana amemvisha cheo na kumwapisha, dkt.Elirehema Doriye(cc) kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa eneo la Mamlaka Ngorongoro (NCAA) na kumwagiza kwenda kusimamia mambo matatu muhimu ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya barabara ndani ya hifadhi hiyo.
Dkt Doriye aliteuliwa na rais Samia Suluhu Hasani Mei 6, Mwaka huu 2024 kuwa kamishna wa uhifadhi Ngorongoro ,akichukua nafasi ya Richard Kiiza ambaye alitenguliwa Machi 15 Mwaka huu.
Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 23 Desemba, 2024 katika viwanja vya makao makuu ya NCAA, Waziri Balozi Pindi Chana amempongeza Dkt Dorie kwa kusimamia ongezeko la mapato ambapo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba, 2024 jumla ya shilingi Bilioni 138,680,341,953.65 zimekusanywa huku watalii 551,512 (Watalii wa nje 350,091 na watalii wa ndani 201,421) wakitembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro katika kipindi cha miezi mitano.
“Nakupongeza kwa juhudi hizi kubwa ulizozifanya katika kipindi cha miezi minne iliyopita, endelea kuongeza juhudi katika usimamizi wa mapato, kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kuimarisha Mahusiano ya kikazi, Usimamizi wa haki za watumishi, mahusiano na wadau na kuongeza hamasa ya Utalii wa ndani ” aliongeza Balozi Chana.
"Pia tumeshuhudia uimarishaji wa mahusiano ya kikazi, umerudisha imani ya watendaji kazi katika Taasisi miongoni mwa watumishi na kutengeneza mifumo mbalimbali ya kitaasisi unaohamasisha kufanyakazi kwa weledi"
"Sisi kama wizara hatuna shaka na uwezo wa CC ambaye leo tumemwapisha na tutahakikisha tunaendelea kutumia vipawa vyake na watumishi wa Ngorongoro mpeni ushirikiano"Alisema.
Aidha waziri Chana alimtaka Kamishna huyo wa uhifadhi kuendelea kuimarisha miundo mbinu ya barabara na madaraja,huduma za maji kwa watalii.
Alitoa maelekezo kwa CC Doriye,kupanua wigo wa watalii na utalii,mamlaka itenge mipango bora ya kuvutia vivutio kama Olduvaigoji ,Mapango ya amboni,Kimondo cha Mbozi,Magovu ya Engaruka nanenwonla Mumba ili kuvutia vivutio vya mambo Kale.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Uhifadhi Ngorongoro, jenerali Venance Mabeyo(Mastaafu), alimpongeza raia Samia Suluhu Hasani kwa kumteu dkt Doriye akidai kwamba mamlaka inaimani kubwa na yeye .
"Kuteuliwa kwako ni ishara ya kuaminiwa,tunaamini uzoefu wako utachangia mafanikio ya NCAA kwani matarajio ni Makubwa, simamia mambo matatu ambayo ni uhifadhi endelevu, kuendeleza utalii na kuhakikisha maendeleo ya jamii" alisema.
Akiongea mara baada ya kuapishwa ,dkt Doriye aliahidi kusimamia uhifadhi endelevu, kuhakikisha rasilimali za asili na kihistoria zinalindwa dhidi ya uharibifu,kusimamia matumizi endelevu ya teknolojia na ushirikishwaji wa jamii katika kutunza nazingira.
Dkt Doriye ambaye pia alimshukuru Rais Samia kwa kumteua,aliahidi kukuza utalii wa kimkakati ,kuimarisha miundo mbinu ya barabara ili Ngorongoro ibaki kuwa taasisi inayoheshimika duniani.
Ends .
0 Comments