DC ACHAFUA HALI YA HEWA BARAZA LA MADIWANI ARUSHA,AWASHUKIA VIKALI WATENDAJI WANAOKWAMISHA MIRADI YA BARABARA ,AAMURU JENGO KUVUNJWA ALIYEPOKEA FEDHA NA KUTOA KIBALI CHA UJENZI KUZITAPIKA!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 



MADIWANI wa halmashuri ya Jiji la Arusha wamechachamaa wakihoji kusuasua kwa  utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara wakati walishaidhinisha fedha kwa ajili ya miradi hiyo, jambo linalowaweka kwenye wakati ngumu wa kujibu  kero hiyo kwa wananchi 

Katika kikao hicho cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025, Mkuu wa wilaya ya Arusha Feliciani Mtahengerwa aliwajia juu wataalamu wa halmashauri hiyo akidai wanachangia kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoamuriwa na baraza hilo.

Dc Mtahengerwa alihoji juu ya fedha zilizotengwa milioni 28 kwa kila kata kutengeneza miundombinu hiyo, na kutaka majibu yenye ufafanuzi kutoka kwa mwenyekiti wa baraza hilo ,jambo hilo ambalo linawakosesha imani na wananchi wao. 

Mkuu huyo wa wilaya pia alihoji matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya uwekaji wa taa katika barabara za ndani za jiji hilo na kueleza kuwa watendaji wa jiji hilo wanabonge la pepo lazima walikemee.
1
Mtahengerwa aliwataka watendaji wote wanaohusika na miradi ya barabara wakiwemo TARURA na Watu wa manunuzi, kuikamilisha kwa wakati vinginevyo wataachia nafasi zao. 

"Nawaambia madiwani muda wenu ni mchache, acheni kuwachekea hawa watawaangushia shimoni, muda ukifika mtaogopa kusimama majukwaani kunadi sera zenu kw sababu ya wazu wazembe wanaopokea fedha na kushindwa kuwajibika ipasavyo, maana wananchi wanawaangalia nyinyi, endeleeni kufumbia macho mambo haya mtaumia"aliongeza

" Kama hizo pesa zimeshatengwa ni miezi mitatu sasa kwa nini changamoto ziko palepale, sitamvumilia yeyote atakayetaka kurudisha nyuma jitihada za serikali" ameeleza Mtahengerwa. 

Hata hivyo amewakumbusha madiwani kusimamia usafi wa mitaa, kuhamasisha ufungaji wa taa za barabarani, kupanda miti na kuibua wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu.

Hata hivyo Mtahengerwa aliwaonya baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo kugeuka madalali wa kuuza maeneo muhimu ya serikali

Katika hatua nyingine Mtahengerwa aliagiza kuvunjwa kwa lengo la biashara linalojengwa katika barabara ya Afrika mashariki ,mkabala na hospitali ya Rufaa Mont Meru akidai kwamba aliyetoa kibali cha ujenzi siku zake zimetimia na kuwaonya baadhi ya madiwani wanaojihusisha na udalali wa kuuza maeneo ya umma.


"Kuna baadhi ya madiwani wamegeuka madalali wa kuuza maeneo ya umma na ninawajua kwa majina yenu na fedha mlizopewa ,ninawaonya acheni hizo tabia,kweli eneo la diplomatic kuna hospitali ya rufaa Mont Meru nyinyi mnafanya udalali  mnatoa kibali cha ujenzi, nimemwagiza inginia hakuna chochote kitakachoendelea ,mtoke hapa mkavunje, na kama mmekula fedha zitawatokea sehemu yoyote ya wazi"








Diwani wa viti maalum Sakina Mpanju, Isaya Doita wa Ngarenaro, Labora Ndarpoi waTemi,   Naboth Silasie wa Lemala ni baadhi ya madiwani waliotaka ufafanuzi kwa nini miradi ya barabara imeshindikana kukamilika kwa wakati ilihali pesa zimeshatengwa. 

Awali akifungua baraza hilo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe amedokeza akiwataka madiwani hao kutojadili suala la barabara kuwa, vifaa vimeagizwa vikifika wataambiwa. 

"Vifaa vimeagizwa nje na vikiletwa tutaitana kuvipokea ili kazi ya matengenezo  ya barabara na mitaro iendelee, bahati nzuri ukusanyaji wa mapato unaenda vizuri, hivyo ni imani yangu kwamba miradi yote  itakamilika kwa wakati" ameeleza Iranqhe.





Ends....

Post a Comment

0 Comments