Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WAHITIMU katika Chuo cha uhasibu Arusha IAA, wametakiwa kutumia tafiti walizopata kuisaidia jamii kukabiliana na changamoto kwenye maeneo waliyoyabaini .
Rai hiyo imebainishwa na Naibu waziri qa Fedha na Mipango Hamadi Chande wakati akimwakilisha Waziri wa fedha ,Dkt.Mwigulu Nchemba kwenye mahafali ya 26 ya chuo hicho ambapo wahitimu 5854 wa ngazi ya astashahada, stashahada,shahada na shahada ya uzamili na cheti walitunikiwa .
Alisema ,endapo watabaki na matokeo ya tafiti hizo watakuwa hawajawasaidia watanzania,kwani itakuwa vema kama wale walioshirikishwa kwenye tafiti zao watapata mrejesho wa kile kilichokuwa kikifanyiwa utafiti ili waweze kufanyia kazi .
“Tafiti zenu zisiishie kwenye maktaba au machapisho baada ya kuhitimu,shirikisheni jamii matokeo ya tafiti zenu yatumike kama.chachu katika kuleta mabadiliko chanya,kuongeza tija kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii ,utendaji kazi wa kila siku katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi ,usimamizi wa taasisi na mashirika, uboreshaji wa sera,mipango na mikakati kwa ustawi wa taasisi, mashirika ,jamii na maslahi mapana ya Taifa.”alisema Chande.
Aidha alisema kuwa, kadri watakavyokuwa waadilifu ,wabunifu,wazalendo na watakapojituma katika kazi watakazoenda kuzifanya katika maeneo mbalimbali kwenye sekta ya umma na binafsi ndivyo watakavyoionesha thamani na tija ya elimu waliyoipata Chuo cha uhasibu Arusha.
Pia aliwataka wahitimu kuwa waaminifu sehemu za kazi, kwani hiyo ni moja ya nguzo ya kupata maendeleo.
Aliupongeza Uongozi wa IAA kwa kuanzisha ushirikiano na Shule ya Polisi Moshi kutoa za kozi za masuala mbalimbali yakiwemo Usalama na amani pamoja na Ulinzi wa taarifa, na kusisitiza kuwa hizi ni kozi za kimkakati zinazoenda kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya ulinzi na usalama.
" Tumeshafanya ziara za kimkakati nchini Comoro, Sudan Kusini, China na Uingereza ili kufanya mazungumzo na baadhi ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya juu kuona namna tunavyoweza kushirikiana katika utoaji wa mafunzo katika viwango vya kimataifa' alisema Prof. Sedoyeka
Aidha, Prof. Sedoyeka alisema IAA ina mpango wa kufungua kampasi mbili za Kimataifa katika nchi za Comoro na Sudani Kusini na wapo katika hatua nzuri ikiwemo kubadilishana walimu na wanafunzi.
Prof. Sedoyeka alisema IAA itaendelea kuanzisha mitaala inayokidhi mahitaji ya Soko la Ajira Kitaifa na Kimataifa na kubabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Naye mwenyekiti wa Bodi ya IAA,Mwamini Tulli amempongeza Menejimenti ya Chuo kwa kuendelea kuandaa wahitimu mahiri, na wenye weledi na kuahidi kuwa kushirikiana nao kulinda hadhi ya Chuo ilijengwa muda mrefu
Ends..
0 Comments