Biteko awaita wadau kuwekeza Kagera
Na Lydia Lugakila
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati mhe. Dotto Biteko amewataka wazawa wa Mkoa wa Kagera wanaoishi nje na ndani ya Nchi kutumia fursa ya Ijuka Omuka ikiwa ni hatua ya kuchochea kukua kwa uchumi hususani sekta ya viwanda na utalii.
Waziri Biteko ametoa wito huo wakati akiongea katika ufunguzi wa kongamano la uwekezaji kupitia tamasha la ijuka omuka lililofanyika katika ukumbi wa KCU uliopo manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera
Tamasha hili la ijuka omuka lenye neno la kihaya la ijuka omuka' lina maana ya kumbuka nyumbani limeandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa pamoja na wadau wa maendeleo Mkoani humo lengo likiwa ni kuwataka wazawa wa Kagera kukumbuka nyumbani na kuwekeza ili kuinua mkoa wa Kagera kiuchumi.
Kwa upande wake Waziri wa mambo ya ndani Innocent Bashungwa alisema wataendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa huo ili kuhakikisha wanasukuma mbele maendeleo ya Mkoa huo huku akiishukuru Serikali kuendelea kuwekeza Kagera huku akimshukuru Rais Samia kwa kuupa nafasi Mkoa huo katika kipaumbele cha miradi mbali mbali ya maendeleo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema tamasha hilo limeza matunda mbali mbali ikiwa ni kuanzisha viwanda vipya na Mkoani humo pamoja na watu wake kujipambanua kiuchumi zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kuendeleza kilimo Tanzania Daktari John Kyaruzi alisema kuwa mradi wa uwekezaji wa vizimba mia nne hamsini tayari umepata muwekezaji kutoka Nchini Marekani.
wakati huohuo mhadhiri wa chuo kikuu Cha sokoine Daktari Philmon Nyinondi akisema tayari taasisi ya tume ya sayansi COSTEC wametenga fedha Kwa ajili ya utafiti wa njia bora ya uvunaji wa senene.
Tamasha hili la pili la uwekezaji la mkoa wa Kagera limezinduliwa Desemba 19,2024 na litaendelea hadi Desemba 26 Mwaka huu.
0 Comments