By Ngilisho Tv
JUMLA ya watoto 38 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya kuzaliwa Yesu Kristo ndani hospital nne kubwa zilizopo Arusha Jana.
Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mount Meru, Dk Ernest Alex amesema katika hospital hiyo walizaliwa watoto saba wakiwemo wakiume wanne na wakike watatu.
Dk Alex amesema kuwa watoto hao wote waliozalowa wako katika afya njema na salama wakiwemo na wazazi wao na muda wowote wataruhusiwa na kwenda majumbani mwao.
Alisema wodi ya wazazi katika hospital hiyo iko na vifaa vyote muhimu ikiwemo huduma safi na ndio maana kwa sasa akina mama wengi huenda kukifungulia katika Hospitali ya Mount Meru.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ngarenaro, DkAntony Mmao amesema kuwa watoto wawili walizaliwa katika hospitali hiyo akiwemo mmoja wa kiume na mwingine wa kike na wote wako katika hali nzuri.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Levolosi, Dk Alex Mjee alisema kuwa jumla ya watoto 13 walizaliwa mkesha wa sikukuu ya kuzaliwa Yesu Kristo juzi ambapo watoto wa kiume walikuwa saba na watoto wa kike walizaliwa sita na wote wako na afya njema pamoja na wazazi wao.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mama na Mtoto ya Kaloleni, Dk Anna Kimaro amesema kuwa jumla ya watoto 16 walizaliwa mkesha wa sikukuu ya kuzaliwa mkombozi Yesu Kristo wakiwemo tisa watoto wa kiume na saba watoto wa kike.
Dk Kimaro alisema kuwa kufuatia uboreshaji na huduma na kuwekwa vifaa tiba vyenye thamani kubwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika hospital hiyo akina mama wengi wamekuwa wakijifungua katika hospitali hiyo na kuacha kwenda hospital Binafsi.
Amesema na kuwakumbusha akina mama kuwa serikali imekuwa ikiwajali na kuwathamani na itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma muhimu na vifaa tiba muhimu vinapatikana katika hospital hiyo ya mama na mtoto lengo la Rais ni kutaka kuwafikishia karibu huduma wananchi.
Ends..
0 Comments