AMUUA MKE KWA KUMCHINJA KISHA KUJIREKODI NA KUPOST MTANDAONI

 AMUUA MKE WAKE KWA KUMCHINJA KISHA KUJIREKODI NA KUPOST MTANDAONI

By Ngilisho Tv

Mwanamume mmoja aliyejuliakana kwa jina la Sbusiso Lawrence nchini Afrika Kusini anadaiwa kumuua Mwanamke ambaye imeelezwa alikuwa Mwenza wake mwenye umri wa miaka 25 kwa kumchinja shingoni na kisha kuchapisha (Post) maiti yake kwenye mitandao ya kijamii na kutengeneza picha mjongeo (video) akikiri kuhusika na mauaji hayo, na sababu ya kumuua.


Mwanamume huyo kupitia Video hiyo ameelezea kuwa amekuwa akimsaidia Mwanamke huyo mtoto ambaye si wake huku uhusiano wao ukiwa kwenye migogoro ya mara kwa mara na kwamba mwanamke huyo alipata fedha kiasi kikubwa na kuanza kumtaka waachane ingali mwanamke huyo alimsababisha Sbusiso kuachana na Mwanamke wake mwingine ambaye alizaa naye kwa usumbufu wa marehemu mpaka kufika wao kurudiana tena ili kulea familia.


Inaelezwa kuwa siku ya tukio walikuwa wametoka kumnunulia mtoto huyo nguo, kisha akamuomba mwenzi wake amsindikize mahali Fulani na ndipo sa walipofika njiani akamvuta msituni na baada ya mabishano yalioendelea baina yo wawili ndipo akafanya kitendo hicho kibaya cha mauaji.


Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na Vyombo vya Habari nchini humo mwanzoni mwa juma hili, vimeeleza kuwa Mwanaume huyo nayeye amejiua kwa kujinyonga na kwamba mwili wake ulikutwa ukining’inia kwenye mti, umbali fulani kutoka pale alipokuwa ameutupa mwili wa mkewe. 


Chanzo - SABC News

Post a Comment

0 Comments