ALBERT MSANDO DC WA KWANZA ANAYEKATWA MSHAHARA WAKE KUWASAIDIA MACHINGA,NI MFANO WA YESU ALIYEKUBALI KUFA MSALABANI KWA AJILI YA WANADAMU

 By Ngilisho Tv

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema anakatwa Tsh.Milioni 2.8 kila mwezi kutoka kwenye mshahara wake wa Tsh. Milioni 3.1 kama rejesho baada ya kukopa Benki kiasi cha Tsh. Milion 106 ili kutengeneza vibanda vya Wamachinga zaidi ya 700.


Hatua hiyo imekuja baada ya Machinga kutaka kujenga vibanda ila hawakuwa na pesa na walipotaka kukopa Benki ili wajenge wakakosa sifa, ndipo DC Msando akaamua akope yeye ili awajengee mabanda Wamachinga hao.


“Nilikaa na Wamachinga wakaniambia Mmachinga akiingia hapa na deni la Laki 2 la kulipia banda hatochomoka maana hata mtaji wa kuuza hana, Benki wakasema wazo la kwanza lilikuwa kujenga banda ambalo Wamachinga watakopea hilo banda litatumika kama dhamana, nikasema Mmachinga kukopeshwa hela hamtompa kwasabbau hana historia ya kibenki , nikawaza tufanyaje na nataka mabanda yakamilike maana yapo nusu, nikaamua kukopa”


“Nilisema Rais aliona inampendeza kuniteua kuwa DC ili niwatumikie Wananchi nikaiomba Benki naomba nikope wengi waliona ni mwehu wengine wananicheka hadi leo kwamba ‘umekopa sababu ya machinga!?’ nikasema ndio” 


“Nikasema badala ya kuchukua pesa kwenda kumpa Mke wangu na Watoto wangu au kupanua biashara zangu, Mimi nitachukua pesa nitamalizia mabanda ili Wamachinga wafanye biashara zao”———Msando

Post a Comment

0 Comments